MWENYEKITI wa Wanawake wajasiriamali soko la sabasaba Anna James, amewaomba wafanyabiashara wa mbogamboga na matunda kutii sheria na maelekezo yanayotolewa na Halmashauri ya jiji la Dodoma ambayo yanawataka kujiepusha na kufanya biashara eneo lisilo salama kwao na bidhaa kwenye stendi ya daladala Sabasaba.
Wito huo umetolewa kufuatia na wajasiriamali hao kufanya biashara kwenye eneo ambalo linatumiwa na madereva wa daladala kupaki magari, ambapo sasa wafanyabishara hao wamekuwa wakipanga biashara zao bila kujali usalama wao,wateja na bidhaa zinazouzwa..
Mwenyekiti huyo alisema hayo alipokuwa akizungumza na wajasiriamali mbele ya Afisa Masoko wa Jiji la Dodoma James Yuna, baada ya kuwatembelea kwa ajili ya kuwaelimisha wafanyabiashara hao ambao wanaofanya shughuli zao za uuzaji wa mboga na matunda kwenye eneo hilo la stendi ya daladala.
Alisema kuwa kwa wafanyabiashara hao hakuna kikwanzo cha kukaidi maelekezo, sheria na. kanuni zilizowekwa na Jiji bali kinachotakiwa ni kuiunga mkono juhudi hizo zinazofanywa kwa ajili ya mpangilio ulio mzuri,hivyo tunatakiwa kukitii kwa vitendo kwa kuondoka na kupisha ili eneo hilo liweze linatumiwa na madareva hao wa daladala kwa uhuru.
Alisema kuwa serikali kupitia Rais John Magufuli ametuwekea malengo wafanyabiashara wote ndogo ndogo ya kuboresha biashara zetu, ambapo hivi sasa vitambulisho tutakavyopewa vitatuwezesha kupatiwa mikopo ili tujiinue zaidi kiuchumi.
"Akina mama ninawaomba tuiunge mkono Halmashauri yetu ya Jiji la Dodoma kwa hili ambalo lipo kwa ajili ya usalama wetu,tuwe tayari muda wote kutoa ushirikiano kwa vitendo na maelekezo yatakayotolewa ikiwemo hili la kupisha eneo hili la stendi ya sabasaba ili daladala ziwe zinafanya kazi yake kwa uhuru na uwazi kwenye eneo hili"alisema.
Kwa upande wake Afisa masoko wa Jiji la Dodoma James Yuna alisema kuwa rai yake kwa wafanyabiashara wa stendi ya sabasaba wanafanya shughuli zao kwa mpangilio, ili kuepukana mwingiliano kati yao na waendesha daladala ambao wamekuwa wakipaki magari yao.
Alisema kuwa mpangilio huo utawasababishia kufanya biashara zao kwa uhuru tofauti na ilivyo kwa vihi sasa ambapo kuna mwingiliano mkubwa unaoweza kusababisha kutokea ajali kwa upande wao na hata kwa wateja ikiwemo na kuharibiwa bidhaa zao wanazoziuza.
Hata hivyo pamoja na zoezi la kuwataka wapishe eneo hilo pia kwa upande wa matolori wachoma mishikaki,mahindi mabicha na wapika chips,ambao wanaofanya biashara hizo katikati ya magari yanayotumia nishati ya mafuta ni hatari kwa upande wao pia.
“Ni rai yangu wafanyabiashara wote kuendelee kutii maelekezo kwa kuwa ni njema inayowataka wanaofanya shughuli zaokuzingatia vigezo vilivyoelekezwa katika kila eneo hivyo tunaomba ushirikiano kutoka kwao’alisema.
Afisa huyo hata hivyo amewataka wafanyabishara kufanya biashara kwa malengo ambayo yatakayowafanya kujiinua kiuchumi na hatimaye kufikia malengo yao.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.