Wafanyabiashara ya uuzaji wa nyama na samaki wamepewa elimu ya afya, sheria na taratibu za uendeshaji wa maduka ya nyama na utumiaji machine za EFD katika Kata ya Viwandani Jijini Dodoma.
Afisa Mtendaji wa Kata hiyo, Tunu Mahamudachi (pichani kushoto) amesisitiza kuwa lengo la kuwaita wafanyabiashara hao ni kuhakikisha biashara wanayoifanya inasimamia usalama wa afya kwa wananchi.
Aidha, Afisa Mifugo wa Kata ya Viwandani Elia Mtamwa licha ya kuwataka wananchi kununua vyama kwenye mabucha ambako ndio sehemu sahihi na salama, amewasisitiza wafanyabiasha kufuata sheria na taratibu za uanzishaji wa mabucha na usafirishaji wa nyama kutoka sehemu moja kwenda sehemu ingine.
Wafanyabiasharaa hao wametoa maoni yao juu yakile walichokipata katika kikao hicho kilichofanyika katika ofisi ya Mtendaji wa Kata ya Viwandani na kuahidi kufanyia marekebisho maeneo yote waliyoshauriwa kitaalam na kwamba watazingatia sheria na usalama wa afya za wateja wao.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.