• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Wazazi Kata ya Uhuru watakiwa kulipa kipaumbele swala la malezi ya watoto

Imewekwa tarehe: May 31st, 2023

Na. Theresia Nkwanga, UHURU

WAZAZI wa Kata ya Uhuru wametakiwa kulipa kipaumbele swala la malezi kwa watoto na kujenga utamaduni wa kuzungumza nao ili kuwalinda dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia.

Kauli hiyo ilitolewa na Diwani wa viti maalum wa Jiji la Dodoma, Fatuma Zollo alipokuwa akiongea na wananchi wa Kata ya Uhuru pamoja na wanafunzi wa Shule ya Msingi Uhuru iliyopo Halmashauri ya Jiji la Dodoma.

Zollo alisema kuwa wazazi wanatakiwa kutenga muda wa kuzungumza na watoto wao ili kusikiliza changamoto zinazowakabili, pia kupunguza ‘ubusy’ wakutafuta pesa na kuelekeza nguvu zao katika kulea watoto. “Wazazi siku hizi tupo ‘busy’ sana, asubuhi tunaenda kutafuta riziki hatuna muda na watoto tumewaachia walimu malezi ya watoto wetu. Watoto wanapitia changamoto nyingi sana, vijana wengi wanawadangaya watoto wetu kwa vitu vidogovidogo kama pipi na biskuti na kuwafanyia vitendo vya ukatili wa kijinsia. Wakati umefika sasa wazazi tuchukue nafasi zetu tuwalinde watoto wetu. Wazazi tutenge muda wakuzungumza nao kama rafiki zetu ili wawe huru kutuelezea changamoto zao” alisema Zollo.

Aidha, aliwaomba watoto kuvunja ukimya pindi wanapofanyiwa vitendo vya ukatili wa aina yoyote ile, kuripoti kwa watu wao wakaribu ili wahusika wafikishwe kwenye mikono ya sheria na kupewa adhabu stahiki. “Watoto msiogope chochote acheni kuficha siri mnavyowaficha wahalifu mnalea maradhi. Ukiona mtu anakugusa sehemu za mwili wako au anakubusu hivyo ni viashiria vya kufanyiwa vitendo vya ukatili msivifumbie macho, toa taarifa kwa walimu, wazazi au nenda Polisi usisubiri hadi ufanyiwe ukatili ndio utoe taarifa” alisema Zollo.

Nae Diwani wa Viti Maalum Jiji la Dodoma, Janeth Kusaduka aliwashauri kina mama kuacha kulinda ndoa zilizojaa manyanyaso na ukatili. Aliwataka kupaza sauti pindi wanapofanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa kuwashtaki waume zao wanaoshiriki vitendo hivyo kwenye madawati ya jinsia, ili waweze kutokomeza matendo ya ukatili wa kijinsia katika ngazi ya familia.

“Kina mama vipigo wanapokea sana ila wanashindwa kushtaki kwa kisingizio cha hatuwezi kulea watoto wenyewe, mwisho wa siku wanaishia kupoteza maisha kwa vipigo na kuwaacha watoto yatima. Ndugu zangu ibada njema inaanzia nyumbani tukiendekeza vitendo hivi watoto wetu tunawafundisha nini? Waume zetu tunawapenda sana lakini ndoa ikiwa ndoano tusikubali kuvumilia matendo ya ukatili tuwashtaki waende wakajifunze” alisema Kusaduka.

Kwaupande wake Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Kata ya Uhuru, Haruna Ngereza aliwashauri watoto kuwa na nidhamu, kutojiingiza kwenye makundi mabaya na kushiriki matendo ya uhalifu kama wizi, ulevi na uvutaji bangi hali inayopelekea kupewa adhabu na kugeuza adhabu hizo kuwa ukatili wa kijinsia.

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.