Na. Dennis Gondwe, CHANG’OMBE
WAZAZI wa Mtaa wa Mazengo Kata ya Chang’ombe wametakiwa kijikita katika malezi ya watoto ili wawe na maadili mema yatakayowawezesha kuwa raia wema na wawajibikaji katika jamii.
Kauli hiyoilitolewa na Afisa Ustawi wa Jamii wa Kata ya Chang’ombe, Debora Kanuya alipokuwa akiongea na wananchi wa Mtaa Mazengo kwenye mkutano wa hadhara ulioandaliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kufanyika katika Ofisi ya CCM Tawi la Chang’ombe Magharibi jijini Dodoma.
Kanuya alisema “ninawaomba sana akina mama wa Mtaa wa Mazengo, tuwe na maneno mazuri kwa watoto wetu ili watoto wanapokuwa wawe wanafahamu maneno mazuri, wasiwe na maneno ya matusi na maneno ya mtaani. Lakini pia kuna baadhi ya akina mama ambao wamekuwa wakipiga sana watoto wao na kutoa lugha ya matusi. Unakuta baadhi ya kina mama wametelekezwa kwa hiyo zile hasira za kutelekezwa wanazihamishia kwa watoto, huo ni ukatili. Niwaombe sana wanawake wenzangu tujikite katika malezi bora ya watoto wetu ili waje kuwa viongozi na raia wema kama sisi. Sisi tusingepata malezi bora tusingekuwa katika nafasi hizi na kuweza kuongea nanyi”.
Aidha, alikemea tabia ya baadhi ya wanawake wanaokunywa pombe kupindukia. “Ndugu zangu kuna akina mama ambao wanakunywa sana pombe. Kinachosikitisha zaidi wanakwenda na watoto vilabuni. Kina mama wengine hawana muda na watoto wao, watoto wanashinda wakiwa wachafu, wakiwa na njaa. Tuwatunze watoto wetu ili baadae pia watutunze” ailisema Kanuya kwa uchungu.
Kwa upande wake Katibu wa Hamasa na Chipukizi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Dodoma, Nasra Seif alisema kuwa jamii inatakiwa kuwalea watoto katika maadili mema ili kuwa na taifa imara lenye watu wanaowajibika. “Siku hizi kumekuwa na tatizo kubwa sana la ukatili wa kijinsia kwa watoto. Twende tukawalee watoto kwa maadili na nidhamu” alisema Seif.
Mkazi wa Chang’ombe, Juma Shaban alisema kuwa changamoto kubwa kipindi hiki ni malezi ya watoto. Watoto wanaanchiwa kujilea na kulelewa na makundi rika jambo linalosababisha kukuwa bila maadili yaliyo mema kwa jamii.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.