WITO umetolewa kwa wazazi, jamii, wadau wa sekta za umma na binafsi kuwatia moyo wasichana/wanafunzi wa kike kuwahimiza kupenda masomo ya sayansi katika kuimarisha mchango wa utafiti na ubunifu wa kisayansi wenye tija kwa ustawi wa uchumi kwa maisha ya kizazi cha leo na kesho.
Kwani hatua hiyo itawezesha kukua kwa viwanda na sekta nyingine za kipaumbele ifikapo mwaka 2025
Akizungumza wakati wa hafla ya maadhimisho ya kimataifa ya siku ya kimataifa ya wanawake na wasichana katika Sayansi,Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Omary Kipanga alisema kuwa ubunifu unaofanywa na wanawake na wasichana unahitajika na unachangia kikamilifu katika ukuaji wa uchumi kwa taifa.
"Uwekezaji unaofanywa na serikali ya awamu ya sita katika miundombinu na rasilimali watu unasaidia kufanyika kwa utafiti wa kisayansi unaolenga kuzalisha ubunifu na teknolojia zinazojibu changamoto za watanzania," alisema Kipanga
Kipanga alisema maadhimisho hayo yanatumika kama sehemu ya kuwahamasisha wasichana na wanawake kuhamasika kusoma masomo ya sayansi, hisabati, uhandisi na ubunifu ili kuongeza namba za wanawake na wasichana katika soko la ajira kwa upande wa Sayansi.
"Siku hii itumike kuwahamasisha wanawake na wasichana kujikita zaidi kusoma masomo ya sayansi, uhandisi, hesabu, ubunifu na teknolojia," alisisitiza Kipanga
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya afya na masuala ya UKIMWI Stanslaus Nyongo amesema pamoja na jitihada kubwa za kuwasaidia watoto wa kike kusoma masomo ya sayansi, bado kuna changamoto ya walimu wa masomo ya sayansi ni wachache.
"Jitihada ni kubwa sana zinazofanywa na Serikali ila bado kuna changamoto kwa upande wa walimu wanaofundisha masomo ya sayansi hivyo ni vyema tukaongeza jitihada katika kuwatengeneza walimu watakaokuja kuwa msaada katika kuwafundisha watoto hawa katika masomo haya ya Sayasi, hesabu, uandisi, na ubunifu," alisema Nyongo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu Prof. Maulilio Kipanyula alisema kuwa, nchi za Afrika ushiriki wa wanawake na wasichana katika masomo ya Sayansi, teknolojia, ubunifu na Hisabati ni asilimia 24 tu. Hivyo, maadhimisho hayo ni sehemu ya kuwahamasisha wanawake na wasichana kushiriki kikamilifu katika masomo ya Sayansi, teknolojia na ubunifu.
"Maadhimisho haya yanatumika kuhamasisha wanawake na wasichana kushiriki kikamilifu katika masomo ya sayasi, teknolojia, ubunifu na hisabati naamini tukifanya hivi hata huko kwenye soko la ajira wataongezeka," alisema Kipa
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.