MWALIMU Mkuu wa Shule ya Msingi Michese Mkoani Dodoma Sizya William amewataka wazazi na walezi kushirikiana na walimu wa shule hiyo katika kuinua ufaulu wa wanafunzi.
Akizungumza na Mtandao wa Dodoma News Blog Mwalimu William amesema kwamba, ili kuongeza ufaulu wa wanafunzi, wazazi wanapaswa washirikiane na walimu ili kujua maendeleo ya wanafunzi kitaaluma.
Aidha amesema kuwa wazazi wengi wamekuwa hawafuatilii maendeleo ya watoto wao shuleni hata wanapoitwa kwenye vikao mbalimbali vya kujadili maendeleo ya kitaaluma shuleni hapo, kwani suala la kukuza ufaulu wa wanafunzi si la walimu pekeyao bali wazazi pia wanapaswa kuwafuatilia watoto wao.
Pia suala la utoro limekuwa tatizo kubwa kwa wanafunzi wa shule hiyo kwani wanafunzi wengi wamekuwa watoro, lakini wazazi wanapoitwa waende kusikiliza wito wamekuwa hawahudhurii, hivyo basi ili kupandisha ufaulu wa wanafunzi ushirikiano mkubwa unahitajika kwa wazazi na walimu.
Pamoja na mwitikio mdogo wa wazazi kutofuatilia kwa ukaribu maendeleo ya wanafunzi uongozi wa shule unafanya juhudi nyingi ili kuhakikisha wanafunzi hawashuki kitaaluma kwani ufaulu wao unazidi kuongezeka siku hadi siku.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.