MWENYEKITI wa dawati la jinsia mkoani Dodoma, Theresia Mdedemi amewaja wazazi na walezi kuwa ni moja kati ya watu wanaofanya vitendo vya ukatili kuongezeka kutokana na usiri na matendo mengi kumalizwa kifamilia hali inayowafanya wahusika wa matendo hayo kuwa sugu.
Aliyasema hayo katika kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliyofanyika kimkoa katika uwanja wa Shule ya Msingi Mkonze wakati akitoa taarifa kwa mgeni rasmi Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Dodoma, Mhe. Felista Bura ambapo alitoa ripoti ya matukio ya ukatili wa kijinsia kwa mkoa wa Dodoma.
Mdedemi alisema kuwa, hiyo ndiyo changamoto kubwa wanayokumbana nayo katika dawati la jinsia na kuonekana kuwa ndio uzio wa kumalizika kwa tatizo la ukatili wa kijinsia, ambapo wazazi, walezi na jamii kwa ujumla wana mtazamo hasi wa kuripoti matukio hayo na kuona kama familia itadharaulika hivyo kuyamaliza majumbani bila ya kuyaripoti polisi katika dawati la jinsia.
“Takwimu za kesi zilizoripotiwa kuanzia Januari hadi Disemba kwa mwaka 2018 ni kesi 1,114. KUbaka kesi 303, kulawiti kesi 76, kukeketakesi 4, kutoa mimba kesi 13, kutelekeza watoto kesi 88, kutelekeza familia kesi 124, shambulio la kudhuru mwili kesi 194, kuzini na maharimu kesi 9, kutorosha wanafunzi kesi 144, mimba kwa mwanafunzi kesi 159.
“Kipindi cha Januari hadi Disemba mwaka 2019, ulikuwa na jumla ya kesi 1,138. Kubaka kesi 191, kulawiti kesi 79, kutoa mimba kesi 10, kutelekeza watoto kesi 58, kutelekeza familia kesi 162, shambulio la kudhuru mwili kesi 254, kuzini na maharimu kesi 3, kutorosha wanafunzi kesi 202, na kumpa mimba mwanafunzi kesi 179” alisema mwenyekiti huyo.
Mbali na changamoto hiyo pia, ametaja baadhi ya visababishi ambavyo vinapelekea ongezeko la takwimu hizo kwa mwaka 2019 tofauti na ilivyokuwa kwa mwaka 2019, kuwa ni pamoja na kushindwa kuyafikia maeneo ya pembezoni.
“Tunashindwa kuyafikia maeneo ya pembezoni kutokana na changamoto za rasilimali fedha na vifaa. Kutokana na hali hiyo tunashindwa kuandaa makongamano, vipeperushi, majarida, na semina ambavyo vingeweza kutusaidia kufikisha ujumbe haraka kwa jamii hali inayopelekea jamii kuwa na uelewa mdogo juu ya makosa ya ukatili, badala yake tunasubiria mialiko kutoka kwa wadau pekee.
“Aidha, ongezeko la wasichana wadogo kupelekwa mijini kwa ajili ya kufanya kazi za majumbani ambapo wengi wao huishia kufanyiwa vitendo wa kikatili. Lakini kutokana na mazingira yanayotumika, wengi hushindwa kuwa wakweli katika kueleza uhalisia wa yale wanayokumbana nayo na mwisho wa siku huishia kuvumilia ili waendelee kukaa mjini. Hivyo niwaombe tu tuvunje ukimya ukifanyiwa ukatili njoo uripoti bila kuangalia aliyekufanyia ni nani”, alisisitiza.
Alimetoa wito kwa wazazi, walezi, wadau jinai na wasimamizi wa sheria wawe makini katika usimamiaji wa sheria zinazomkandamiza mwanamke, na kuhakikisha wote wanaohusika katika ukiukaji wa sheria hizo kukamatwa, kufunguliwa mashtaka, kuhukumiwa na kuadhibiwa kisheria kwa mujibu wa sheria ili iwe fundisho kwa wenye tabia za kukiuka na kuzivunja sheria kwa kutekeleza ukatili wa kijinsia.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.