Na. Dennis Gondwe, MNADANI
WAZAZI na walezi wametakiwa kufuatilia maendeleo ya watoto wao katika masomo kila siku ili kufahamu tabia na mienendo ya watoto wao.
Kauli hiyo ilitolewa na Diwani wa Viti maalum Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Janeth Kutona alipokuwa akiongea na wananchi wa Kata ya Mnadani jijini Dodoma.
Kutona alisema “tumekuja kutoa darasa kwa ajili ya kizazi hiki. Ndugu zangu wazazi na walezi, watoto wetu wanaosoma shule tujitahidi sana kufuatilia maendeleo yao kwa kukagua madaftari, kufuatilia tarehe ya kila siku husika. Utaratibu huu utamsaidia mzazi kujua kama mtoto wake ni mtoro au la. Tusiwe ‘busy’ sana na kazi za uzalishaji mali, tujali kwanza watoto wetu ndio tuendelee na uzalishaji mali. Elimu hii tunaomba muifikishe kwa wenzenu ambao leo hawajafika. Pia mtakapokuwa na mikutano yenu mtualike ili tutoe elimu hii kwa upana zaidi”.
Madiwani 14 wa Viti maalum wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma wanafanya ziara katika kata 41 za jiji hilo kutoa elimu dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia katika jamii na fursa za kiuchumi.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.