Na Sifa Stanley, Dodoma
WAZAZI wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma washauriwa kutoa elimu ya afya ya uzazi kwa watoto wao ili kuepusha madhara yatokanayo na ukosefu wa elimu hiyo.
Hayo yalisemwa na Mratibu wa Afya ya Uzazi na Vijana, Fidea Obimbo wakati wa kikao cha afua ya afya ya uzazi na maendeleo ya vijana kilicho fanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma alipokuwa akitoa takwimu zinazohusu afya ya uzazi hususani kwa kinamama na vijana.
Akielezea kuhusu faida ya elimu ya afya ya uzazi kwa watoto alisema kuwa, elimu ya afya ya uzazi kwa watoto itawasaidia watoto kujitambua na kuwa na uelewa wa masuala yanayohusu jinsia na namna ya kukabiliana na changamoto watakazo kumbana na kuwasilisha changamoto hizo kwa wazazi wao. “Nilianza kuongea kwa uwazi na watoto wangu kuhusiana na masuala yanayohusu ngono katika umri mdogo wakiwa darasa la tatu, lazima tupige mbiu kwa wazazi watoe elimu kwa watoto” alisema Obimbo.
Naye Mratibu miradi wa Shirika la Kiota Women Health and Development (KIWOHEDE) Said Mwemezi alisema kuwa shirika lao linajihusisha na utoaji wa elimu ya afya kwa vijana na watoto, hususani elimu kuhusu balehe ili kuwasaidia watoto hao kuwa na uelewa wa masuala ya afya na kuongeza kuwa shirika linatoa kondomu bure kwa vijana ili waweze kujikinga na magomjwa ya zinaa.
Akieleza juu ya umuhimu wa elimu ya afya ya uzazi kwa kwa watoto ambao ni wanafunzi na vijana, Afisa uraghibishaji wa shirika la DODOMA YOUTH DEVELEPMENT ORGANIZATION (DOYODO) Hawa Ally alisema kuwa, huduma ya elimu ya afya ya uzazi kwa watoto ni muhimu kwasababu inawapa watoto uwanja wakuelezea matatizo yao ya kiafya kwa uwazi na kusaidika kwa uharaka. Aliongeza kuwa shirika la DOYODO limetoa mchango wa kutoa huduma hiyo mashuleni. “Tumeanzisha vyumba vya afya ya uzazi mashuleni ambapo unahifadhi taulo za kike kwaajili ya mabinti pia tunatoa huduma ya elimu ya afya ya uzazi kwa vijana waliopo mashuleni” alisema Ally.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.