WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Innocent Bashungwa amemhakikishia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kuwa ujenzi wa miundombinu ya huduma za afya katika hospitali za Wilaya, vituo vya afya na zahanati zote nchini utakamilika kwa wakati na kwa ubora zaidi ili wananchi waendelee kupata huduma bora za afya kwa wakati.
Bashungwa amesema kuwa kufuatia maelekezo yaliyotolewa na Mhe. Rais kuwa hataki kuona majengo ya hospitali yaliyomalizika kujengwa hayatumiki na badala yake yanabaki kuwa maboma, OOfisi ya Rais - TAMISEMI inaenndelea kutekeleza maagizo hayo akisisitiza kuwa ukamilishaji wa majengo hayo ya vituo vya afya unaambatana na ununuzi wa dawa, vitendanishi na vifaa tiba pamoja naa ajira za watumishi watakaotoa huduma katika vituo hivyo.
Hayo yamesemwa leo tarehe 8 Juni, 2022, katika ziara ya Rais Samia Wilayani Biharamuro, Mkoani Kagera.
"Mhe. Rais ulituagiza Ofisi ya Rais - TAMISEMI kuwa hutaki kuona majengo ya hospitali yanabaki kuwa maboma, lakini pia ulituelekeza ujenzi wa hospitali hizi, vituo vya afya na zahanati lazima ukamilike ili wananchi wapate huduma, nikuhakikishie Mhe. Rais ujenzi wa miundombinu hii itakamilika kwa wakati na ubora zaidi" amesema Bashungwa.
Aidha, Waziri Bashungwa amemshukuru Mhe. Rais kwa kuwekeza fedha kwa ajili ya uboreshwaji wa miundombinu ya kutolea huduma za afya ya msingi, barabara na miundombinu ya elimu ya msingi katika Halmashauri ya Wilaya ya Biharamuro, Bashungwa amesema mindombinu hii inakwenda kuboresha maisha ya wananchi wa Biharamuro na Mkoa wa Kagera kwa ujumla.
Kwa upande mwingine, Bashungwa amesema kutokana na maelekezo aliyotoa Mhe. Rrais kuhusiana na zao la Buni ambalo kwa asilimia kubwa linalozalishwa Mkoani Kagera, maelekezo hayo yameleta matumaini makubwa kwa wakulima na wafanyabiashara wa zao hilo kwa kuwa bei ya buni imepanda hadi kufikia shilingi 3,720 kwa kilo.
"Muelekeo uliotoa Mhe. Rais katika zao la kahawa, matumaini ni makubwa, mwaka jana ulifanyika mnada wa zao la buni aina ya Radika limeuzwa kwa bei ya 3,720 haijapata kutokea" alisisitiza Bashungwa.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.