• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Waziri Aweso aridhishwa uchimbaji wa visima Dodoma

Imewekwa tarehe: December 21st, 2020

WAZIRI wa Maji Mhe Jumaa Aweso amefanya ziara ya kushtukiza usiku kukagua zoezi la uchimbaji wa visima vya maji pembezoni mwa jiji la Dodoma alivyoagiza kuchimbwa ili kutatua changamoto ya upatikanaji wa maji safi katika jiji la Dodoma.

Akizungumza akiwa kwenye mradi huo Mheshimiwa Aweso amesema ameamua kufanya ziara hiyo kuona kama agizo lake la uchimbwaji visima usiku na mchana kama linatekelezwa.

“Sote tunatambua tuna upungufu wa maji katika jiji letu na katika ziara yangu na Katibu Mkuu katika Mamlaka ya DUWASA niliagiza kuchimbwa kwa visima vya dharura na vichimbwe usiku na mchana, nimekuja kuona hilo nashukuru zoezi linaenda vizuri” amesema Mhe Aweso.

Aidha amemuagiza Katibu Mkuu Wizara ya maji Mhandisi Antony Sanga kuhakikisha anasimamia zoezi hilo sambamba na kuongeza uchimbwaji visima vingine viwili ili kufikia idadi ya visima vitatu kupunguza tatizo la maji katika Jiji.

Pia ameitaka Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Mkoa wa Dodoma DUWASA kuhakikisha wanasimamia vyema mgawanyo wa maji kwa wananchi kwamba licha ya upungufu wa maji lakini kila mwananchi ni lazima apate sababu ndio uhai wa binadamu.

Amesema Serikali inampango kabambe wa kuhakikisha inatatua tatizo la maji katika Mkoa wa Dodoma ambapo tayari wamelipa fidia tayari kwa ujenzi wa bwawa kubwa la Farukwa  litakalokuwa kama chanzo cha maji na wapo katika taratibu za kufikisha maji yanayotoka ziwa Victoria.

Aidha ametoa onyo kali kwa wataalamu wa maji katika Wizara, Mamlaka za Maji na Halmashauri kuwa mda wa janjajanja umekwisha yeyote atachukuliwa hatua atakapoonekana kizembea kwenye nafasi yake kwani ilani ya chama inaonyesha wananchi wanatakiwa kupata huduma ya maji.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya maji na usafi wa mazingira Mkoa  wa Dodoma Mhandisi Aron Joseph amesema kisima hicho kina urefu wa mita 150 na sasa mkandarasi amefikia urefu wa mita 40 na kinatakiwa kukamilika ndani ya siku 30.

Amesema kwa sasa Jiji la Dodoma kutokana na ongezeko la watu kunahitaji mita za ujazo 103000 lakini zinazozalishwa kwa sasa ni mita ya ujazo elfu 66 hivyo jitihada kubwa zinahitajika kumaliza tatizo la maji katika jiji la Dodoma.

Naye Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Antony Sanga amesema wizara tayari imetoa shilingi bilioni moja kwa ajili ya uchimbwaji wa visima pembezoni mwa jiji la Dodoma ili kukabiliana na tatizo la maji.

Amesema kisima hicho ni kikubwa kina milimita 400 ambazo ni sawa na nchi 16 na kitawekewa pampu kubwa ya kupampu maji huku akibainisha kuwa kama Wizara watatenga fedha nyingine kwa ajili ya kuongezwa kwa visima vingine viwili katika eneo hilo.


Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.