WAZIRI wa Ujenzi, Innocent Lugha Bashungwa (Mb) amefungua Mkutano wa sita wa Mafundi sanifu ukiwa na kauli mbiu Matumizi ya Akili Mnemba kuongeza ufanisi: Kuwaimarisha Mafundi Sanifu kwa Changamoto zinazoibuka” leo Mei 23,2024 jijini Dodoma.
Mkutano wa sita wa mafundi safinu ambao umewakutanisha takribani mafundi sanifu 800 kutoka sehemu mbalimbali nchini. unalenga kuwajengea uzoefu katika kufanya kazi kwa kutumia mapinduzi ya teknolojia, yaani akili mnemba.
Akifungua mkutano huo Msajili wa Bodi ERB Mhandisi Bernard Kavishe, ameeleza kuwa Bodi imeandaa miradi mbalimbali kwa ajili ya kuwawezesha mafundi sanifu kufanya kazi kwa vitendo hususani kwa wale wanaomaliza vyuo vikuu, huku miradi hiyo inatarajiwa kuzinduliwa mwezi Septemba, 2024.
Aidha, amewataka Mafundi sanifu wote nchini kuendelea kujisajili katika Bodi ya ERB kama yalivyo matakwa ya Sheria ili waweze kutambulika na kupata mazingira wezeshi katika fursa mbalimbali za miradi ya ujenzi inayoendelea hapa nchini ambapo amesisitiza kuwa idadi ya mafundi sanifu 2,785 iliyopo hivi sasa ni ndogo ikilinganishwa na wanaohitimu kila mwaka.
Pia, Bashungwa ametoa wito kwa Mafundi sanifu kuhakikisha ujuzi walionao usiishie kwenye Karakana zao kwa ajili ya maonesho bali warasimishe na kuingiza sokoni ili uweze kutatua matatizo yaliyopo kwenye jamii kuwawezesha kupata kipato na kuendeleza vipaji vyao kwa kuanzisha kampuni zitakazochangia uchumi wa Taifa.
Amesisitiza umuhimu wa uadilifu katika kufanya kazi, maadili na miiko ya taaluma ya Kihandisi na kuwa tayari kuripoti wote ambao wanakiuka maadili ya uhandisi ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya Sheria.
Katika mkutano huo Waziri Bashungwa alishuhudia kiapo cha waandisi wapya 48.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.