• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Waziri Bashungwa aiagiza COSOTA kuhusu mirahaba, wasanii kuula

Imewekwa tarehe: September 11th, 2021

WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa ameigiza Taasisi ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA) kuandaa mpango mkakati wa makusanyo ya mirabaha pamoja na takwimu za maeneo yanayotakiwa kulipa mirabaha na kuziwasilisha wizarani mwisho mwa mwezi Septemba.

Waziri Bashungwa ametoa agizo hilo leo jijini Dodoma katika kikao chake na Kikosi kazi cha kukusanya maoni ya wadau katika Kanuni ya Leseni na Maonesho kwa Umma ya 2021 kutoka COSOTA kikiwasilisha taarifa ya maoni ya wadau kwa kanuni hiyo.

"Katika kikao ambacho tutakutana baada ya wiki mbili hizi mje na mkakati huo lazima tujue tunakusanya kwa akina nani na wako wapi pamoja na idadi yao, pia ongezeni kasi ya ukusanyaji wa mirabaha Disemba tunatakiwa kutoa gawio kubwa," alisema Mhe. Bashungwa.

Amesisitiza kuwa anahitaji kupata makadirio ya makusanyo ya mirabaha hiyo kwa mwaka huu wa fedha na kuanzisha utaratibu ambao atakuwa akifuatilia hali ya makusanyo hayo kwa kila mwezi kwa kuhakikisha anapata taarifa.

Pamoja na hayo naye Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Pauline Gekul aliitaka COSOTA kuhakikisha inajipanga zaidi na kujenga utaratibu wa kushirikiana na mashirikisho na vyama vinavyosimamia maeneo ya kukusanya mirabaha ili kutengeneza mazingira rafiki ya zoezi hili la ukusanyaji.

Aidha, Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi alifafanua kuhusu suala la kukamilika kwa mfumo utakao kuwa ukihesabu na kutambua nyimbo zinazochezwa katika vituo vya Redio kuwa unatarajia kukamilika mwezi Oktoba na ndiyo utaanza kufanya kazi rasmi.

"COSOTA mna kazi kubwa ya kufanya na kuhakikisha mnakusanya fedha za kutosha ili gawio la mwezi Disemba liwe lenye hamasa kwa Wasanii wetu ni imani yangu kuwa kwa Kanuni hii mpya na viwango hivi mlivyopanga kuwa vinalipika, kikubwa katika hili ni kuweka mifumo ya kiteknolojia ambayo itarahisisha makusanyo hayo,"alisema Dkt. Abbasi.

Chanzo: Na Anitha Jonas - COSOTA, Dodoma

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.