WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima amekabidhi mitungi ya gesi kwa wanawake 1000 iliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Dkt. Gwajima amekabidhi mitungi hiyo yenye thamani ya sh. milioni 72 wakati akifungua Kongamano la Wanawake viongozi wilaya ya Mkuranga, mkoani Pwani Disemba 15, 2023
Amesema nia ya kutoa mitungi hiyo ni kuwawezesha wanawake kutumia nishati safi ili kujinasua na changamoto za kiuchumi zinazochangiwa pia na kutafuta nishati kwa gharama kubwa na muda mwingi kwani Rais Samia amedhamiria kuwakomboa wanawake kwa vitendo.
Aidha, Waziri Dkt. Gwajima amefafanua kuwa nia ya Serikali kuwawezesha wanawake ni kuwafanya waimarike kiuchumi ili kusaidiana na wanaume kuanzia ngazi ya familia huku akiwakumbusha kila jinsi kutimiza majukumu yao katika nafasi zao.
Amebainisha kuwa, kutokana na Mkutano wa Wanaume wa kutokomeza Ukatili uliofanyika Afrika ya Kusini hivi karibuni, Tanzania inaanzisha makongamano ya wanaume na yatazinduliwa katika wilaya ya Mkuranga mwakani 2024.
Dkt Gwajima, amempongeza Mbunge wa Mkuranga Abdalah Ulega, Waziri wa Mifugo na Uvuvi, kwa jinsi anavyoshirikiana na uongozi wa Wilaya hiyo na kufanya mabadiliko makubwa kwenye kuchochea wananchi kujiletea maendeleo. Ameongeza Pongezi pia kwa Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Hadija Nasri kwa umoja na mshikamano wa viongozi katika Wilaya yake hali iliyowezesha uratibu mzuri wa Majukwaa ya Uwezeshaji wanawake kiuchumi.
Dkt. Gwajima amesema utaratibu wa kukutana kila mwaka kujadili mada mbalimbali za kijamii ni matokeo ya uongozi wa kimkakati ambapo wilaya hiyo ni mfano wa kuigwa katika katika uundaji wa Majukwaa hayo nchini.
Vilevile Waziri Dkt. Gwajima amewakumbusha wanawake kujiunga na Vikundi vya Ujasiriamali vilivyosajiliwa ili kuingia kwenye Majukwaa ya Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi.
Kwa upande wake Mhe. Abdallah Ulega amesema kitendo cha Rais Samia kutoa mitungi hiyo ya Gesi wilayani humo ni ishara ya Rais kuwa kinara wa kuwakomboa wanawake
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.