• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Waziri Gwajima asisitiza tahadhari zaidi ya magonjwa

Imewekwa tarehe: February 25th, 2021

SERIKALI imewataka viongozi wa Serikali, sekta binafsi, Viongozi wa Kijamii na Viongozi wa Dini wa Madhehebu mbalimbali kuacha kusubiri matamko zaidi bali waamke na kuwajibika katika nafasi zao katika kutoa elimu kwa wananchi juu ya kujikinga na magonjwa mbalimbali ya mlipuko katika maeneo yao.

Hayo yamebainishwa leo Februari 24, 2021 Jijini Dodoma na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima wakati akitoa tamko la Serikali lenye lengo la kuongeza kasi katika kuchukua tahadhari ya kujikinga na magonjwa ya mlipuko na magonjwa katika mfumo wa hewa.

Dkt Gwajima amesema imefika wakati kwa kila kiongozi katika nafasi yake kuendelea kutoa tahadhari juu ya namna ya kujikinga na magonjwa mbalimbali badala ya kusubiri serikali itoe tamko.

“Mheshimiwa Rais na Waziri Mkuu wameshafanya kazi kubwa na nzuri ya kutoa matamko ya kukumbusha na kuelimisha taifa juu ya mwelekeo wa tahadhari za kuchukua ili kuepuka mlipuko wa ugonjwa wa COVID-19. Vilevile, Viongozi wa Wizara ya Afya tumetoa matamko mbalimbali ya kuwakumbusha na kuwaelimisha wananchi kuchukua tahadhari” amesema Dkt Gwajima.

Dkt Gwajima amesema jukumu la kinga dhidi ya magonjwa yote yakiwemo ya kuambukiza na yasiyoambukiza ni la kila mtu katika nafasi yake  kuhakikisha wanachukua tahadhari kujikinga na magonjwa hayo.

Ameongeza kuwa “niwakumbushe viongozi wa Serikali na sekta binafsi, Viongozi wa Kijamii, Viongozi wa Dini wa Madhehebu mbalimbali ngazi zote  tuache kusubiri matamko zaidi bali tuamke tuwajibike kila mmoja kwa nafasi yake” amesema.

Amebainisha kuwa kila mwaka katika kipindi cha Novemba hadi Machi wimbi la magonjwa  yanayoathiri mifumo ya upumuaji na chakula  huongezeka kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa huku ikiwatoa wasiwasi Wananchi kuendelea kuchukua tahadhari.

Magonjwa hayo yanaweza kusababishwa na vimelea vya bakteria, virusi na fangasi huambukiza kutoka kwa mtu mmoja kwenda mwingine kwa njia mbalimbali ikiwemo hewa, kula au kunywa kitu ambacho siyo kisafi na salama.

“Mwenendo huu wa magonjwa ni kila mwaka na kipindi hiki  tumeshuhudia Dunia ikipambana na wimbi la pili la mlipuko wa ugonjwa wa COVID- 19,kwa msingi huu tunahitaji kuongeza kasi zaidi ya kuchukua tahadhari dhidi ya mwenendo huu wa magonjwa yote haya kwenye kipindi hiki” amesema

Dkt Gwajima amesema ni vyema wakafanya ufafanuzi tena juu ya mambo muhimu ya kuzingatia katika kutekeleza hatua za tahadhari za kujikinga na magonjwa ya kuambukiza na milipuko kwa ujumla wake ikijumuisha na tahadhari dhidi ya tishio la mlipuko wa COVID-19.

Amesema kwanza wananchi wanatakiwa kuondoa hofu  zinazojengwa bila sababu na nia njema,  kwa sababu hofu inaleta madhara zaidi kiafya.

“vifo vingi vinavyotokea duniani asilimia 90 hutokea kwasababu watu wanatanguliza hofu  zaidi,”amesema

Aidha Dkt Gwajima amewataka wananchi  kuendeleza tabia ya kunawa mikono mara kwa mara kwa maji safi tiririka na sabuni, iwapo maji tiririka na sabuni hakuna, wanatakiwa kutumia  vipukusi (sanitizer).

Dkt Gwajima ameongeza kuwa “Namuelekeza mfamasia mkuu wa serikali kuendelea kutoa elimu ya jinsi gani tunaweza kutengeneza vipukusi vyetu vya ndani ya nchi  ili kuwezesha wananchi kupata kwa bei nafuu ambayo kila mwananchi ataweza kuimudu” amesema .

Aidha amemuelekeza mfamasia mkuu wa serikali kutangaza orodha ya watengenezaji wa barakoa ambao tumeshawathibitisha, pia elimisha jinsi ya kutengeneza barakoa binafsi. vaa barakoa kwa kuzingatia muongozo uliotolewa na wizara hususan katika maeneo ya msongamano.

Pia amesema kila mwananchi anatakiwa kufanya  mabadiliko ya tabia ya lishe anayotumia kwa kuhakikisha unapata lishe bora ikiwemo matunda na mbogamboga kwa gharama nafuu kulingana na mazingira ya vyakula vya asili katika eneo lako.

“Naelekeza wataalamu wa lishe ngazi zote kuandaa daftari la orodha ya vyakula vya asili vinavyopatikana eneo husika na kutoa elimu ya milo ipi iandaliwe kama kielelezo cha lishe bora. tuache kuamini kuwa lishe bora ni vyakula vya kisasa vya biashara na vya bei ghali,” amesema.

Kwa msaada wa Fullshangwe Blog

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.