Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo amekabidhi pikipiki 23 kwa Watendaji wa Kata, maafisa mipango miji na afisa mifugo wa jiji la Dodoma mara baada ya kuhudhuria kikao cha Baraza la Kufunga mwaka cha Jiji la Dodoma.
Pikipiki hizo 23 zimegharibu jumla ya shilingi 54,900,000 ambazo zimetoka kwenye mapato ya ndani ya Halmashari ya Jiji.
Aidha Waziri Jafo amelipongeza Jiji la Dodoma kwa utendaji kazi bora ambao umesababisha mabadiliko makubwa katika utoaji huduma kwa wananchi wa Dodoma. "Haya ni matunda ya ushirikiano mzuri wa utendaji kazi kati ya madiwani na watendaji wa Jiji la Dodoma, hongereni sana Dodoma" alisema Jafo.
Akimkaribisha Waziri Jafo kwa ajili ya kukabidhi pikipiki hizo, Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Godwin Kunambi alisema, Jiji la Dodoma limedhamilia kuhakikisha linatoa huduma bora na kwa wakati kwa wananchi wake. Lakini pia pikipiki hizo zitasaidia kupunguza changamoto ya usafiri kwa watendaji wake.
Mkurugenzi Kunambi alifafanua kuwa "...pikipiki hizi unawakabidhi Maafisa Watendaji wa Kata 20 zilizo pembezoni mwa jiji letu ili kuwawezesha maafisa hao kuwafikia wananchi kwa wakati na kupunguza kero ya usafiri kwenye maeneo ya mbali. Pikipiki 2 ni kwa ajili ya Maafisa wa Mipango Miji kitengo cha Uthibiti wa Ujenzi holela na moja utaikabidhi kwa Afisa Mifugo anayehusika na udhibiti wa wanyama wanaozurura hovyo mjini", alisema.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo (Mb) akikabidhi funguo za pikipiki kwa Diwani wa Kata ya Zuzu Mhe. Awadh Abdallah kwa niaba ya Mtendaji wa Kata ya Zuzu wakati wa hafla ya kukabidhi pikipik kwa Watendaji wa Kata 20 za pembezoni mwa Jiji, Maafisa Ardhi kitengo cha Udhibiti wa Ujenzi holela (2) na Afisa Mifugo (1) kwa ajili ya udhibiti wa wanyama wanaozurura hovyo mjini.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.