• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Waziri Jafo aridhishwa na barabara Hospitali ya Uhuru, atoa maelekezo Mji wa Serikali

Imewekwa tarehe: March 8th, 2021

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Selemani S. Jafo (Mb), ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa barabara inayoingia Hospitali ya Uhuru kwa kiwango cha lami yenye urefu wa Mita 320 kwa njia mbili ambayo inasimamiwa na Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) katika Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma.

Waziri Jafo alitoa pongezi hizo alipokuwa akifanya ziara ya ukaguzi wa miradi mbalimbali mkoani Dodoma Machi 03, 2021 na kuonesha kuridhishwa na kasi ya ujenzi wa barabara hiyo.

“Tumejenga Hospitali ya Uhuru lakini sehemu hii ya kuingilia ilikuwa na changamoto kubwa, nimekuja hapa kuangalia maendeleo ya ujenzi wa barabara hii na kwa kweli nimeridhika kuona maendeleo ya ujenzi wa barabara hii”, alisema Mhe. Jafo.

Aidha Mhe. Jafo alimtaka Mkandarasi anayetekeleza ujenzi wa barabara hiyo M/S Nyanza Co. Ltd kutumia muda uliopo ili kuweza kukamilisha mradi kwa wakati kutokana na changamoto za mvua zinazoendelea kunyesha.

Akitoa taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa barabara hiyo, Meneja wa TARURA Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino Mhandisi Nelson Maganga alisema kuwa ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha lami umefikia asilimia 85 na tayari lami nyepesi imekamilika kwa ajili ya kuweka tabaka la lami nzito.

“Ujenzi wa barabara umefikia asilimia 85 kukamilika na tunatarajia Mkandarasi kumaliza kazi kulingana na mkataba kufikia Machi 14, 2021, sehemu hii ya barabara imegharimu kiasi cha shilingi Milioni 511”, alisema Mhandisi Nelson.

Katika hatua nyingine Mhe. Jafo alifanya ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa Barabara za Mji wa Serikali Mtumba kwa kiwango cha lami zenye urefu wa Km 51.2 na kuonesha kutoridhishwa na kasi ya Mkandarasi anayetekeleza ujenzi wa barabara hiyo Kampuni ya China Heinan International Cooperation Co. Ltd (CHICO) na kumtaka Mkandarasi huyo kuhakikisha anamaliza ujenzi kama ilivyo kwenye mkataba ifikapo Julai 30, 2021.

“Sijaridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa mradi huu kuwa chini kwa asilimia 6, leo hii mpo asilimia 63 na mlitakiwa muwe asilimia 69 mimi nilikuja hapa nikijua mpo asilimia 70, sihitaji mjadala wa aina yeyote ninachotaka mradi huu uwe umekamilika kama ilivyo kwenye makubaliano”, alisema Mhe Jafo.

Akitoa taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa Barabara za Mji wa Serikali Mtumba, Mkurugenzi wa Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini - TARURA, Mhandisi Mohamed Mkwata alisema kuwa mkandarasi amefikia asilimia 63 za maendeleo ya jumla ya utekelezaji wa mradi ambapo alitakiwa kuwa asilimia 69, ameongeza kuwa ujenzi wa tabaka la lami umefikia Km 11.2, uwekaji wa lami nyepesi Km 15.7, ujenzi wa tabaka la pili umefikia Km 15.7, ujenzi wa tabaka la kwanza umefikia Km 15.7, ujenzi wa mifereji Km 6.6, pamoja na ujenzi wa vivuko 64 dhidi ya 130 vinavyohitajika.

Aidha, Mhandisi Mkwata alieleza kuwa katika kipindi cha mwezi Novemba 2020 uhaba wa saruji pamoja na mvua zinazoendelea kunyesha zilisababisha baadhi ya kazi kusimama na kufanya mkandarasi kuwa nyuma kwa asilimia 6 za utekelezaji wa mradi na kuongeza kuwa ili kufidia muda uliopita mkandarasi ameongeza mitambo ili kuweza kumaliza mradi huo kwa wakati uliopangwa.

Mhe. Jafo amefanya ukaguzi katika Barabara ya Mji wa Serikali Mtumba ikiwa ni ziara yake ya tatu kukagua maendeleo ya ujenzi wa barabara hiyo inayosimamiwa na TARURA na mradi unatarajiwa kukamilika ifikapo tarehe 30 Julai, 2021.

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.