WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Selemani Jafo amezitaka Halmashauri zote nchini kuhakikisha kuwa kila moja inatekeleza mkakati wa Taifa wa kupanda zaidi ya miti milioni 270 ambapo kila Halmashauri ina jukumu la kupanda miti milioni 1.5 ikiwemo ya kivuli na ya matunda.
Ametoa kauli hiyo wakati wa hafla ya uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti kwa shule vyuo vyote nchini iliyofanyika katika viwanja vya shule ya sekondari Dodoma na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Naibu Waziri wa TAMISEMI anayeshughulikia Elimu David Silinde pamoja na asasi, wanafunzi wa shule mbalimbali na wadau wanaojishughulisha na masuala ya Mazingira.
Alisema kwa sasa dunia inakabiliwa na athari za mabadiliko ya tabia ya nchi hivyo ni wakati muafaka wa kuhakikisha kuwa lengo la kupanda idadi hiyo ya miti linafikiwa.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Silinde aliahidi kusimamia utekelezaji wa shule zote nchini kupanda miti, huku mkuu wa mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka akitoa wito kwa kila mwanafunzi kuhakikisha anapanda mti wake na kuutunza hadi utakapokuwa mkubwa badala ya kuitelekeza.
Naye Meya wa Jiji la Dodoma Mstahiki Prof. David Mwamfupe alisema miti ina faida kubwa tatu ikiwemo kuvyonza sumu kwenye mazingira hivyo utekelezaji wa kampeni hiyo hatua muhimu kwa jamii.
Kampeni hiyo inaongozwa na kauli mbinu isemayo “Soma na Mti” kwani na mahususi kwa wanafunzi wa shule na vyuo.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.