WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Seleman Jafo aipongeza Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa utendaji kazi wa viwango katika ukusanyaji mapato na utoaji huduma kwa wananchi kwa mwaka wa fedha 2018/2019.
Pongezi hizo amezitoa alipokuwa akitoa salamu zake katika mkutano wa mwaka wa Baraza la Madiwani lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma.
“Niwashukuru sana ninyi viongozi, Madiwani wa Baraza la Madiwani la Jiji la Dodoma, ninyi mmekuwa watu wa mfano, kwa kuthubutu kusimamia Halmashauri yenu, Halmashauri yenu leo hii ime‘graduate’. Leo hii mmehama kutoka kwenye unyafuzi wenu wa mapato, choka mbaya sasa mmefikia shilingi bilioni 71 haijawahi kutokea nchini. Ni ‘outstanding performance’” alisema Waziri Jafo.
Halmashauri maana yake ni kushauriana. “Naomba niwaambie kitu, hapa mmekusanya shilingi bilioni 71 ni sawasawa na Halmashauri nyingine takribani 30. Mnaweza kuzichagua Halmashauri mbili mkawatekelezea miradi yao ya maendeleo yote na mkawalipa mishahara yao na ‘per diem’ zote. Kama leo Halmashauri yenye ‘total’ bajeti ya shilingi bilioni 30, ninyi mnakusanya shilingi bilioni 71, hamjahudumia Halmashauri mbili?” alihoji Waziri Jafo.
Waziri Jafo aliwapongeza watendaji wa Halmashauri hiyo kwa kusimamia ukusanyaji wa mapato, na kusema hajawahi kuona watendaji wazuri kama hao. “Katika Halmashauri ambayo ninajivunia sana, Dodoma ni Halmashauri ya kwanza ambayo ninajivunia sana. Endeleeni na kasi hiyohiyo ya kukusanya mapato” alisema Waziri Jafo.
Aidha, aliwataka Madiwani kuwatia moyo watendaji wa halmashauri hiyo. “Waheshimiwa madiwani endeleeni kuwatia moyo watendaji hawa. Hawa ni binadamu kama binadamu wengine. Ninafahamu yawezekana wengine wanamapungufu, tuwanyooshee vidole wale wenye mapungufu. Lakini wale wazuri tuwape moyo. Tutengeneze timu moja ya kushinda hapa Dodoma” alisema Waziri Jafo.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.