• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Waziri mavunde asisitiza miradi mikubwa ya madini iliyopewa leseni kuanza kazi haraka

Imewekwa tarehe: March 31st, 2025

Na. Mwandishi Wetu, DODOMA

Waziri wa Madini, Anthony Mavunde, ameagiza miradi mikubwa na ya kati ya Madini ambayo tayari imekwishapewa leseni kuanza utekelezaji wake mara moja ili kuchochea ukuaji wa sekta na kuleta manufaa kwa taifa na kutimiza azma ya serikali kutoa leseni hizo.

Waziri Mavunde alisema serikali inataka kuhakikisha kuwa miradi yote ya uchimbaji Madini iliyopangwa kuanza inaanza mara moja bila kucheleweshwa, na kuwa serikali kwa upande wake imejitahidi kurahisisha taratibu kwa wawekezaji na sasa ni wakati wa sekta binafsi kuchukua hatua kwa upande wao.

“Serikali imefanya kazi yake, tumeondoa vikwazo vingi na kurahisisha utaratibu. Sasa ni jukumu la wawekezaji kuhakikisha kuwa miradi inaanza kutekelezwa mara moja” alisema Waziri Mavunde.

Aidha, Waziri Mavunde aliahidi kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na wadau wa madini, ikiwemo TCM, katika kutatua changamoto zinazowakabili wawekezaji ili kuhakikisha sekta hiyo inaendelea kukua kwa kasi na kufikia lengo la uchangiaji wake katika Pato la Taifa (GDP) na maendeleo ya kiuchumi kwa ujumla.

“Sisi kama serikali tutakaa pamoja na taasisi husika ili kuangalia changamoto zilizopo na kuzitatua kwa haraka. Hatutaki ukiritimba wowote ambao unaweza kuchelewesha maendeleo ya sekta hii muhimu, serikali hii ni moja na ina lengo moja” alisisitiza Mavunde. 

Kwa upande mwingine, Waziri Mavunde alisisitiza umuhimu wa utafiti katika sekta ya Madini, akieleza kuwa maendeleo endelevu yanategemea uwekezaji mkubwa katika tafiti zinazosaidia kuongeza uzalishaji na tija. Aidha, amepongeza juhudi za wadau wa sekta hiyo katika kutekeleza Maono ya Vision 2030; Madini ni Maisha na Utajiri inayotekelezwa na Wizara kwa lengo la kuongeza maeneo yaliyofanyiwa utafiti wa kina, kuongeza ajira kwa Watanzania, Miradi ya Uwajibikaji wa Kampuni kwa Jamii (CSR), na uwezeshaji wa Watanzania kupitia Ushirikishwaji wa Watanzania (Local Content).

Kuhusu mchango wa Sekta ya Madini kwenye uchumi wa taifa, Waziri Mavunde ameeleza kuwa Sekta hiyo imeendelea kukua kwa kasi, ambapo mwaka 2022/23 ilichangia asilimia 7.2 ya Pato la Taifa, huku mwaka 2023/24 mchango wake ukifikia asilimia 9.0. Serikali inalenga Sekta hiyo ichangie angalau asilimia 10 ifikapo mwaka 2025, kama ilivyoainishwa kwenye Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2020-2025 pamoja na Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2025.

Katika ukusanyaji wa Maduhuli ya Serikali, Waziri Mavunde amesema mapato yameongezeka maradufu, ambapo mwaka wa fedha wa 2015/16 yalikuwa shilingi bilioni 162, lakini kufikia mwaka wa fedha 2023/24 yaliongezeka hadi shilingi bilioni 753 ambapo kwa mwaka huu wa fedha wa 2024/25, Serikali inalenga kukusanya shilingi trilioni 1, lengo ambalo linaonekana litafikiwa kulingana na mwenendo wa ukusanyaji mapato.

Kwa upande wake, Mtendaji wa Chemba ya Migodi Tanzania (TCM) Mhandisi Benjamin Mchwampaka aliipongeza serikali kupitia Wizara ya Madini kwa kuendelea kuwashirikisha katika hatua mbalimbali za majadiliano kwa lengo la kuweka mazingira rafiki kwa uwekezaji nchini.

Alisema kuwa, Tanzania ni moja ya nchi chache ambazo sekta binafsi inapewa nafasi ya kushiriki vikao muhimu sambamba na Maafisa wa Serikali akitolea mfano ushiriki wa pamoja wa Wizara na TCM katika mikutano mikubwa kama Mining Indaba ambayo hufanya Afrika Kusini kila mwaka.

Chanzo: Fullshangwe Blog


Comments


Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.