WAZIRI wa Madini, Mhe Anthony Mavunde (Mb) juzi tarehe 11 Septemba 2024 Jijini Dodoma amefanya kikao cha pamoja na wachimbaji wadogo na wafanyabiashara ya madini chini ya mwamvuli wa FEMATA na kueleza baadhi ya mikakati ambayo ataipa kipaumbele katika utekelezaji wa majukumu yake.
Mavunde ameainisha dira ya VISION 2030 Madini ni MAISHA na UTAJIRI na kuainisha yafuatayo:_
Kufanya Utafiti wa Jiolojia ya miamba nchi nzima ifikapo 2030 kupitia teknolojia ya kisasa “HIGH RESOLUTION AIRBORNE GEOPHYSICAL SURVEY”.
Ujenzi wa maabara ya kisasa ya jiosayansi ya uchunguzi wa sampuli za miamba, udongo, maji, makinikia, nk.
Uanzishwaji wa makumbusho ya madini.
Uwezeshwaji wa wachimbaji wadogo kupitia STAMICO kwa huduma ya mashine za uchorongaji 15.
Kuongeza ushiriki zaidi wa watanzania kwenye sekta ya madini (Local Content).
Madini ya kimkakati(_critical minerals_) kuwekewa nguvu zaidi ili kukidhi mahitaji ya dunia ya matumizi ya nishati safi.
Uongezaji thamani wa madini hapa nchini.
Kuweka mazingira rafiki ya uwekezaji mkubwa ili kuvutia wawekezaji wa ndani na nje.
Kuimarisha mifumo ya udhibiti wa utoroshaji madini.
Kuongeza mchango wa sekta ya madini katika mauzo ya bidhaa nje ya nchi ili kuongeza upatikanaji wa fedha za kigeni.
Kusimamia ukusanyaji wa mapato (maduhuli) yatokanayo na madini kufikia Trilioni 1 kwa mwaka wa fedha 2023/24.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.