• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Waziri Mkuu aagiza Wakuu wa Wilaya kukutana na wafugaji

Imewekwa tarehe: December 27th, 2022

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameagiza Wakuu wa Wilaya kuitisha vikao na wafugaji ili kujadiliana na kuweka namna bora ya kufanya shughuli za ufugaji ikiwa ni pamoja na kutambua mifugo yote iliyoko ndani ya Wilaya husika na kuweka zuio la mifugo mingine kuingizwa katika wilaya zao.

 Majaliwa pia ameagiza viongozi katika mikoa na wilaya kuweka mpango wa matumizi bora ya ardhi kwenye maeneo yote yenye wafugaji na wakulima ambapo pia kuna vyanzo vya maji.

Amesema kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anataka kuona uharibufu wa vyanzo vyote vya maji vinadhibitiwa kwa kuwekewa mpango mkakati utakaowezesha kuyatunza maeneo hayo dhidi ya uharibifu wa aina yeyote.

Amesema hayo leo Jumamosi (Disemba 24, 2022) wakati akiongoza kikao cha pamoja na Mawaziri wa Kisekta, Makatibu na Naibu Makatibu wakuu kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa na Wilaya za Morogoro wadau na wasimamizi wa masuala ya ardhi na mifugo ili kutatua, changamoto za usimamizi wa masuala ya ardhi ndani ya Mkoa huo.

Kikao hicho kimefuatia maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyoyatoa Desemba 22, 2022 Wakati akifunga njia ya kuchepusha maji na kuanza ujazaji maji kwenye bwawa la kuzalisha umeme la Julius Nyerere (JNHPP).

“Agizo la Mheshimiwa Rais ni lazima litekelezwe kwa sisi wasaidizi kutimiza wajibu wetu na kuweka mikakati ya kutekeleza agizo hilo kwa ufanisi.”

Katika hatua nyingine Mheshimiwa Majaliwa amewataka wakuu wa Wilaya kuunda kamati za maridhiano baina ya wafugaji na wakulima, ili kutengeneza umoja kati ya makundi hayo mawili “Wafugaji washirikishwe kuandaa miundombinu ambayo wanyama wao wataitumia kupata malisho, maji pamoja na majosho”

Aidha, Waziri Mkuu amekemea vitendo vya rushwa kuanzia kwenye ngazi ya viongozi wa Serikali za vijiji “unakuta kiongozi wa kijiji anaruhusu wafugaji kutoka maeneo mbalimbali kwasababu tu amepewa rushwa na anasahau athari ambazo wanazipata wanavijiji wao”

“Jambo lingine muhimu tutambue maeneo yote ya vyanzo vya maji, pamoja na kutambua maeneo ambayo ng’ombe wanaingia katika maeneo ya vyanzo vya maji na kuwaondoa wote ili maji yaendelee kutirika kuelekea katika bwawa la umeme”

Waziri Mkuu amekubaliana na maombi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro la kuwaondoa wafugaji walioko katika eneo la mto kilombero ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Mheshimiwa Rais Dkt.Samia.

Awali, akizungumza katika kikao hicho Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Fatma Mwasa amesema hali ya usimamizi wa ardhi na vyanzo vya maji kwa Mkoa wa Morogoro si ya kuridhisha kwani maeneo mengi ya vyanzo vya maji yameathirika hivyo zinahitajika jitihada za haraka kunusuru hali hiyo.

“Maeneo ya madakio ya maji ya mto kilombero hadi sasa yameathirika kwa asilimia 80 na asilimia 20 iliyobaki ndio inayotegemewa kuzalisha maji katika mto huo tusipochukua hatua sasa hali itakuwa mbaya zaidi.

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.