WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Makatibu Tawala wa Wilaya zote Tanzania Bara watekeleze majukumu yao kwa kuzingatia utawala bora, miiko na maadili ya viongozi wa umma.
“Kila mmoja akazingatie utumishi wa umma unaongozwa kwa misingi ya sheria, kanuni, taratibu na miongozo mbalimbali ya Serikali. Misingi hiyo, ndio chachu ya ujenzi wa taswira nzuri ya Serikali ya Awamu ya Sita.”
Alitoa maagizo hayo wakati akifungua semina elekezi kwa Makatibu Tawala wa Wilaya katika ukumbi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Dodoma.
Pia, Waziri Mkuu amewasisitiza viongozi hao wahakikishe wanadhibiti matumizi mabaya ya fedha za umma katika maeneo yao na wanapobaini kuwepo kwa ubadhirifu wasisite kuchukua hatua.
Waziri Mkuu alisema ili viongozi hao waweze kutekeleza majukumu yao ipasavyo wanatakiwa waweke mikakati namba ambavyo wilaya zao ya zitakavyoweza wilaya kubeba na kusimamia vizuri ajenda za kitaifa.
Kwa upande wake, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene amesema lengo ya mafunzo hayo ni kuwaongezea weledi viongozi hao ili kuimarisha utawala bora.
Naye, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Angela Kairuki amewataka viongozi hao watimize majukumu yao ipasavyo na wahakikishe wanasimamia utekelezaji wa maagizo ya viongozi katika maeneo yao ya kazi.
Awali, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete alitoa wito kwa viongozi hao wahakikishe mafunzo wanayopatiwa wanakwenda kuyafanyia kazi katika maeneo yao.
Mafunzo hayo ya siku tatu yameandaliwa na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa kushirikiana na Taasisi ya Ungozi yamehusisha Makatibu Tawala wa Wilaya 135 za Tanzania Bara.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.