Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Mei 21, 2021 amekabidhi jumla ya magari 184 kwa Maafisa Elimu wa Halmashauri ikiwa ni mkakati wa Serikali ya awamu ya sita ya kuendelea kuboresha sekta ya elimu nchini, hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Shule ya Sekondari Kibasila, Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika tukio hilo, Waziri Mkuu amezitaka Halmashauri zilizopokea magari zizingatie taratibu za serikali katika matumizi na matengenezo ya magari hayo na kuhakikisha magari hayo yanatumika kwa malengo yaliyokusudiwa.
“Maafisa Elimu na Wakurugenzi wa Halmashauri magari haya mmekabidhiwa tukute gari limepaki kisa limekosa ‘Service’ utakuwa umekosa kazi, lazima tuambiane ukweli, magari haya lazima yafanye kazi kwa zaidi ya miaka mitano hadi sita”
Amesema kuwa magari hayo ni kwa ajili ya Maafisa Elimu wa msingi wa Halmashauri zote 184 za Tanzania Bara. Na kwamba, Serikali ya Awamu ya Sita itaendelea kusimamia mchakato wa ununuzi wa magari mengine 184 yatakayogawiwa kwa Maafisa Elimu Sekondari wa Halmashauri zote pamoja na magari matatu kwa utekelezaji ngazi ya Wizara.
Naye, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI Ummy Mwalimu amesema magari hayo yamenunuliwa na Serikali kupitia Programu ya Lipa Kulingana na Matokeo katika Sekta ya Elimu (EP4R) kwa gharama ya shilingi bilioni 16.4.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.