WAZIRI MKUU Mhe. Kassim Majaliwa amekabidhi magari ya wagonjwa 20 yenye thamani ya shilingi Bilioni 2.24 ambayo yatapelekwa kwenye vituo vya afya 13, hospitali za Halmashauri tano, ya wilaya moja na ya rufaa ya mkoa moja katika mikoa 17.
Akikabidhi magari hayo leo Jumanne, Juni mosi, 2021 katika hafla iliyofanyika ofisini kwake Mlimwa, Jijini Dodoma, Waziri Mkuu amezitaka Halmashauri zitenge fedha za matengenezo (motor vehicle services) ili kuhakikisha magari hayo yanadumu kwa muda mrefu zaidi”, amesema.
Amewaomba Wabunge waliopokea magari hayo wakayasimamie ili yatoe huduma inayotarajiwa kwa wananchi, “Msisite kuyaeleza haya masuala kwenye mabaraza ya madiwani ili wahusika wazingatie jukumu la kuyatunza,” amesisitiza Majaliwa.
Amesema mwaka jana alikabidhi magari 50 ya kubebea wagonjwa kati ya 70 yaliyokuwa yamepangwa kutolewa ili kuboresha huduma za afya nchini.
“Mheshimiwa Rais Samia ameridhia magari haya yatolewe na yaende yakatoe huduma kwa wananchi. Pia ameridhia hospitali za mikoa na wilaya ziwe na magari ya kubebea wagonjwa na kuwaleta kwenye huduma kwa haraka.
Kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya uongozi thabiti wa Mama yetu mpendwa Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu ninatoa shukrani za dhati kwa ufadhili huu wa magari haya ambayo yatatumika kuboresha huduma za afya kwa wananchi.” Alimalizia Waziri Mkuu.
Mapema akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza na Wabunge waliofika kupokea magari hayo, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Dorothy Gwajima alisema magari hayo 20, yatapelekwa kwenye hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga, hospitali ya wilaya ya Masasi, hospitali za Halmashauri tano na kwenye vituo vya afya 13.
Alisema magari matano yamepelekwa kwenye hospitali za Halmashauri za Mkalama (Singida), Ngorongoro (Arusha), Chunya (Mbeya), Buhigwe (Kigoma) na Nyamwaga iliyoko Tarime mkoani Mara.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.