WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewaagiza Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi,Vijana, Ajira na Wenye ulemavu, Jenista Mhagama, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwingulu Nchemba, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Tixon Nzunda wakutane ili wakamilishe tarativu za utoaji wa mitambo ya ujenzi wa kiwanda cha sukari cha Mbigiri.
Ametoa maagizo hayo leo Jumamosi, Agosti 14, 2021 baada ya kupokea taarifa ya ujenzi wa kiwanda hicho, wakati alipotembelela mradi wa shamba la miwa la Mkulazi pamoja na kukagua ujenzi wa kiwanda cha sukari Mbigiri, mkoani Morogoro, katika taarifa hiyo Waziri Mkuu alielezwa kuwa kuna baadhi ya mitambo ya ujenzi wa kiwanda imekwamba bandarini.
“Tunataka kiwanda hiki kiane kujengwa, uchelewweshwaji usio na umuhimu hatuupi nafasi, hatukaki ujenzi ukwame, zile kontena 21 kule bandarini tunataka zitoke Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Waziri wa Fedha na Mipangao na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu mkae mkokotoe kile kinachopaswa kulipwa kijulikane mitambo ile itoke.”
Waziri Mkuu amesema kwa namna nchi hii ilivyojipanga katika ujenzi wa viwanda, Tanzania itakuwa na viwanda saba vya sukari lengo likiwa ni kuhakikisha inajitosheleza kwa kuwa na sukari ya kutosha na kuondoa pengo la tani 70,000 ililopo, hivyo kupungiza uagizaji wa bidha hiyo kutoka nje ya nchi.
Mbali na maagizo hayo, pia Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuipongeza Bodi ya Mkulazi, watendaji wa shamba la miwa la Mkulazi pamoja na uongozi wa kiwanda cha Sukari cha Mbingiri kwa usimamizi mzuri wa mradi huo kutokana na hatua kubwa ya maendeleo iliyofikiwa.
Chanzo: owm_tz (instagram)
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.