• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Waziri Mkuu awataka Wakuu wa Wilaya na Waganga wakuu kusimamia maadili ya utumishi sekta ya Afya

Imewekwa tarehe: January 8th, 2023

WAZIRI  Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka wakuu wa wilaya na waganga wakuu wa mikoa na halmashauri zote nchini kusinamia maadili kwa watumishi wa sekta ya afya ili fedha zinazotolewa kwenye sekta hiyo ziendane na ubora wa huduma zinazotolewa kwa watanzania.

Amesema Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameendelea kuhakikisha anatoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya afya, ununuzi wa dawa na vifaa tiba, hivyo dhamira yake hiyo ni lazima iendane na ubora wa huduma zinazotolewa wa watumishi katika sekta ya afya.

Ameyasema hayo wakati akizungumza na viongozi wa Serikali wa mkoa wa Ruvuma, kwenye ukumbi wa Mikutano wa Manispaa ya Songea.

Pia, amewaagiza wakuu wa wilaya kusimamia upatikanaji wa dawa kutoka Bohari Kuu ya Dawa (MSD)  kwani Rais Dkt. Samia anatoa fedha za ununuzi wa dawa “Hatutaki kusikia malalamiko, Serikali kila mwezi inaleta fedha za ununuzi wa dawa, wakuu wa wilaya simamieni hili.”

Katika Hatua nyingine, Waziri Mkuu amewataka Wakuu wa wilaya kwa kushirikiana na Wakurugenzi na Maafisa Elimu kusimamia dhamira ya Mheshimiwa Rais. Dkt. Samia ya kutoa elimu bila malipo kaunzia darasa la awali hadi kidato cha sita kwa kutembelea katika shule na kukagua fomu za kujiunga na shule na kujiridhisha hakuna michango ya hovyo.

Aidha, ameagiza kuwepo na usimamizi wa shughuli za ustawi wa jamii ikiwemo masuala ya kiuchumi na wafanyabiashara wadogo, wakati na wakubwa. “Ni lazima tusimamie mwenendo wa uchumi kwenye jamii zetu, shughuli ambazo zinawaingizia kipato wananchi lazima tuzisimamie na kuziimarisha, lazima tufanye tathimini kama tunafanya vizuri au la, na lazima tujikite kwenye maeneo yote ikiwemo vijijini.”

Kadhalika, Majaliwa amesema viongozi katika halmashauri zote nchini ni lazima waweke utaratibu na kujikita katika kuondoa kero za wananchi pamoja na kuwa na dhana ya ushirikishwaji kwa kuwaeleza kila kinachofanyika Serikalini kwa kutumia vyombo vya habari na kufanya mikutano. “Lazima tufahamu kero zao na  kuzitatua.”

Akizungumza kuhusu makusanyo kwenye Halmashauri nchini Waziri Mkuu ameagiza kufanyike utambuzi wa vyanzo vyote vya mapato na kiasi cha fedha kinachoingia na kuwataka wenyeviti wa halmashairi zote nchini na Mameya kuliwekea nguvu eneo la makusanyo.

Pia ameelekeza kuwa fedha zote zinazokusanywa katika vyanzo vyote ni lazima zipelekwe benki kabla ya matumizi. “Ni muhimu pia kukagua matumizi ya vyombo vyetu ya ukusanyaji wa mapato, fanyeni tathmini za mara kwa mara ya mwenendo wa makusanyo.”

Kwa upande wake, Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt. Festo Dugange amesema kuwa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia analeta fedha nyingi kwa ajili ya utekelezaji wa huduma za jamii na miradi ya maendeleo katika halmshauri hivyo viongozi katika maeneo hayo wanapaswa kusimamia fedha hizo. “Tunapaswa kusimamia na ni wajibu wetu kufanya hivyo ili tulete matunda yaliyokusudiwa na dhamira ya Rais kwa  Watanzania iweze kufikiwa”







Matangazo

  • Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Kwanza 2023December 14, 2022
  • Orodha ya Waliopangwa kwenye Vituo vya Kazi Kada za Afya (Awamu ya Pili) Agosti 2022August 30, 2022
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA KWA KADA ZA AFYA (Marudio)July 20, 2022
  • TANGAZO LA KAZI - TOAJuly 22, 2022
  • MAJINA YA WALIOPATA AJIRA KADA ZA AFYA NA UALIMUJune 26, 2022
  • ORODHA YA WAKUU WA KITENGO CHA FEDHA YENYE MABADILIKO 5-5-2022May 06, 2022
  • Angalia zote



Taarifa Mpya

  • TAASISI ZA SERIKALI KUPITISHWA KWENYE MFUMO WA UKUSANYAJI WA MAPATO WA MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA

    January 09, 2023


  •  
  • VIONGOZI WA ELIMU MSIKAE OFISINI FUATILIENI UFUNDISHAJI NA UJIFUNZAJI MASHULENI- DKT. DUGANGE

    January 09, 2023


  •  
  • WAZIRI MKUU AWATAKA WAKUU WA WILAYA & WAGANGA WAKUU KUSIMAMIA MAADILI KWA WATUMISHI YA AFYA

    January 08, 2023


  •  
  • BILONI 1.5 ZIMEPELEKWA MBINGA, UJENZI WA HOSPITALI YA WILAYA -DKT. DUGANGE

    January 07, 2023


  • Angalia zote




Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.