WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewatoa hofu wawekezaji wanaozalisha bidhaa mbalimbali nchini baada ya kuwaeleza kuwa Serikali itahakikisha inawalinda na kulinda bidhaa zao ili waweze kuata masoko hapa nchini na hata nje ya nchi.
Majaliwa ameyasema hayo leo Jumanne, Aprili 27, 2021 alipotembelea kiwanda cha kuunganisha mabasi cha BM Motors kinachomilikiwa na Mtanzania Bwana Jonas Nyagawa na kiwanda cha madawa cha Kairuki, vilivyopo Kibaha mkoani Pwani na amesema kuwa ameridhishwa na uwekezaji huo.
Waziri Mkuu amesema Serikali imeweka mazingira mazuri ya uwekezaji kwa lengo la kuinufaisha nchi pamoja na muwekezaji. Hivyo, ametumia fursa hiyo kuwakaribisha wawekezaji kuwekeza nchini katika sekta mbalimbali.
“Serikali tupo na nyie, maamuzi tuliyofanya ya kuweka mazingira wezeshi ni maamuzi sahihi, tutapita kusikia changamoto za kila mmoja wenu na kuzitatua, ongezeni mitaji kwenye uwekezaji wenu, tumieni taasisi za fedha kuongeza mitaji” amesisitiza Waziri Mkuu.
Pili, Waziri Mkuu ameziagia taasisi zote za Serikali zinazohusika na masuala ya uwekezaji zihakikishe wawekezaji wote walioonesha nia ya kuwekeza nchini wanasaidiwa na kufanikisha mchakato huo bila ya usumbufu wa aina yoyote.
“Taasisi zote zinazohusiana na uwekezaji zihakikishe kila ambako panatamaniwa na muwekezaji hduma muhimu zipatikane iwe maji, umeme, barabara na hata viwanja vipatikane kwa urahisi.”
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.