WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amesema serikali imedhamiria kuliongeza zao la zabibu kuwa miongoni mwa mazao ya kimkakati ili kungeza thamani zao hilo na kuongeza tija kwa wakulima.
Waziri Mkuu amesema hayo leo Julai 5,2021 jijini Dodoma wakati wa ziara ya kutembelea na kukagua shughuli katika Kituo cha Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) Makutopora, Shamba na Kiwanda kidogo cha Mvinyo kilichopo Msalato,skimu ya umwagiliaji na kiwanda cha CETAWICO Hombolo, Dodoma.
Majaliwa amesema kuwa dhamira ya serikali ni kuwainua wakulima kupitia zao hilo.
‘Serikali imedhamiria kuliongeza zao la zabibu kuwa miongoni mwa mazao ya kimkakati ili kungeza thamani zao hilo na kuongeza tija kwa wakulima”amesema Mhe.Majaliwa
Pia Waziri Mkuu amewaeleza wakulima wa zabibu kuwa Serikali imedhamiria kuboresha kilimo cha zao hilo kwa sababu kilimo ni mkombozi kwa Watanzania.
“Serikali imeanzisha kampeni ya kuhamasisha kilimo cha zao la zabibu, tunataka kumsaidia mkulima kuanzia maandalizi ya shamba, upatikanaji wa pembejeo hadi hatua ya mauzo.”
Amesema kuwa kampeni hiyo itaanzia mkoa wa Dodoma kwa kuwa imegundua kwamba zabibu ni fursa ya kiuchumi nchini na ardhi yote ya wilaya za mkoa wa Dodoma inakubali kilimo hicho.
Aidha Waziri Mkuu amezitaka taasisi za kifedha ikiwemo Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) ibadilike na kutoa mikopo kwa wakati.
Kwa upande wake Mkulima wa zabibu wa Chama cha Ushirika cha mradi wa umwagiliaji wa zabibu Wazamah July Sombe ameelezea changamoto walizonazo wakulima wa eneo hilo ni pamoja na miundombinu ya barabara kufika eneo hilo, ugumu wa upatikanaji wa mitaji kutokana na taratibu ndefu za mikopo za mataasisi ya kifedha, uchakavu wa miundombinu ya umwagiliaji pamoja na riba kubwa ambazo ni vigumu kwa wakulima kumudu na kuendeleza kilimo hicho kwa uzalishaji mkubwa.
Aidha, mkulima huyo ameiomba Serikali kuimarisha masoko ya zao la zabibu kwa kuhamasisha wawekezaji zaidi kununua zao hilo ambalo bado upatikanaji wa soko ni changamoto.
Pia ameongeza kuwa kwasasa mkulima anazalisha tani 4-5 ya zabibu ambayo ni chini ya kiwango kinachoshauriwa na wataalamu cha Tani 15-20.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.