WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Ummy Mwalimu ameagiza Halmashauri ambazo zimekusanya mapato chini ya asilimia 75 ya makisio yake kufanya tathmini na kuhakikisha inaweka mikakati Madhubuti ya kufikia malengo yao ifikapo Juni, 2021.
Waziri Ummy ameiagiza Mikoa kuendelea kusimamia, kutoa ushauri na maelekezo kuhusu suala zima la ukusanyaji na matumizi ya mapato ya ndani ya Halmashauri kabla ya viongozi wa juu kubaini matatizo ya Halmashauri nchini.
Amezielekeza Halmashauri zote nchini kuzuia na kudhibiti matumizi ya fedha mbichi kabla ya makusanyo hayajapelekwa benki, kwa kuwa kwa mujibu wa sheria, fedha inatakiwa kukusanywa na kupelekwa benki ndipo kuanza kutumika.
Aidha, Waziri Ummy amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri kuacha kutumia fedha mbichi za makusanyo kabla ya kupelekwa benki na atakayekiuka hatua kali zitachukuliwa dhidi yake kwa kuwa atakuwa amekiuka miongozo ya kifedha inayomtaka kuhakikisha wanakusanya na kupeleka benki ndipo kuanza kutumika.
Ameitaka Mikoa kuendelea kusimamia Halmashauri kwa kutoa taarifa kupitia mifumo ya kielektroniki, kusisitiza usuhuhishi wa taarifa na usahihishaji wa takwimu katika mifumo mbalimbali na kuongeza jitihada katika usimamizi wa ukusanyaji wa mapato ya ndani katika Mamlaka za Serikali za Mitaa.
Vile vile, amezitaka Sekretarieto za Mikoa kuhakikisha wanatoa ushauri stahiki kwa wakati, kutatua changamoto zilizopo katika suala zima la ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri wanazoziongoza, kutoa miongozo kwa lengo la kuhakikisha Mamlaka za Serikali za Mitaa zinafanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato ili kuleta maendeleo kwa wananchi.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.