WAZIRI wa Afya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ummy Mwalimu akabidhi vifaa tiba vya Afya vyenye thamani ya shilingi Milioni 45 mkoani Dodoma vifaa vilivyotolewa kupitia mradi wa kuboresha huduma Jumuishi za Kifua kikuu, Malaria na UKIMWI kwa Wajawazito kabla na baada ya kujifungua.
Zoezi la ugawaji wa Vifaa Tiba vya Afya lilifanyika katika kituo cha afya cha Makole kuwakilisha vituo vingine 19 ambavyo vinashiriki katika mradi huu.
Mwalimu alisema kuwa vipimo hivyo ni muhimu kwa wajawazito ili kuweza kuepusha kifafa cha mimba na vifo kwa wajawazito
“Niwapongeze Chuo Kikuu cha Dodoma kwa kushirikiana na Liverpool School of Tropical Medicine chini ya ufadhili wa Global Fund na Takeda Pharamaceuticals kwa vifaa hivi. Najua mama wajawazito mpo hapa niwaombe mkifika kwenye Kliniki za Uzazi, Mama na Mtoto mhakikishe mnapimwa wingi wa damu, mkojo kuangalia wingi wa protini, shinikizo la damu pamoja na kusikilizwa mapigo ya moyo ya mtoto bila kutoa gharama zozote vifaa vipo, Serikali ya awamu ya sita imehakikisha upatikanaji wa dawa za kuzuia kutoka damu wakati wa kujifungua, dawa za kuongeza damu na dawa za kuzuia kifafa cha mimba katika vituo vya afya vya umma nchini’’.
Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma Prof. Lughano Kusiluka, alimpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa jinsi anavyotoa kipaumbele kwenye masuala ya Afya.
"Napenda kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya katika kuimarisha huduma za Afya katika nchi yetu na hasa katika eneo hili la mama na mtoto. Katika miaka miwili ya utekelezaji wa mradi huu inaoneshwa kwamba mradi umepokelewa vizuri na matokeo yake yameanza kuonekana kwenye kiwango cha ubora". Prof Kusiluka
Aidha, Mtafiti Mkuu wa Mradi Dkt. Leonard Katalambula alieleza kua wanakusudia kuongeza idadi ya vituo vya afya, kuongeza idadi ya mikoa, kuongeza idadi ya vifaa tiba kwa vituo vitakavyo kuwa katika mradi na vilevile kuwa na kituo cha pamoja cha mafunzo kwa vitendo kwa watumishi walioko kazini.
Mradi wa kuboresha huduma jumuishi za TB,UKIMWI na Malaria ni mradi wa miaka miwili unaofadhiliwa na mfuko wa Global Fund na Liverpool School of Tropical Medicine kwa kutoa mafunzo kwa watoa hudumaza afya ya mama kabla,wakati na baada ya kujifunguaili kupunguza vifo vinavyotokana na uzazi.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.