WAZIRI wa Afya Ummy Mwalimu amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu-Umoja wa Viongozi wa Malaria Afrika Joy Phumaphi.
Katika mazungumzo yao Waziri Ummy ametoa shukrani Kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kutoa msaada wa kifedha na kiufundi kwenye kadi za alama za malaria, Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele (NTDs), Lishe, Huduma ya afya ya uzazi, mama, mtoto na vijana (RMNCAH) na kwa kuboresha ubora wa huduma kwa kutumia kadi ya alama za jamii.
Pia, Mwalimu amemjulisha Katibu Mkuu huyo kuwa Baraza la Kukomesha Malaria litazinduliwa mwezi huu wa Aprili wakati wa kuadhimisha Siku ya Malaria Duniani.
"Ili kuhakikisha mambo yanasonga, tumeanza kumshirikisha Mwenyekiti wetu Mteule Mhandisi Leodgar Tenga katika shughuli mbalimbali ili apate taarifa za kazi zinazotarajiwa za MC," alisema Waziri Mwalimu
"Tanzania tunaamini kuwa mtu yeyote anayekutembelea tena ni rafiki wa dhati, hakika ni mishara ya moyo wa kuendelea kujitolea na ushirikiano kati ya ALMA na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia Wizara ya Afya," alisema Mwalimu
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.