WAZIRI wa Afya Ummy Mwalimu akiongozana na Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Tumaini Nagu wametembelea Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Dar Group Jijini Dar Es Salaam kuona hali ya utoaji huduma katika Hospitali hiyo ambayo sasa ipo chini ya usimamizi wa Taasisi ya JKCI
Waziri Ummy amepongeza uongozi wa Taasisi ya JKCI chini ya Mkurugenzi Mtendaji Dkt. Peter Kisenge pamoja na Watumishi wote kwa kuanza kufanyia kazi maboresho ya ubora wa utoaji huduma za matibabu katika Hospitali hiyo katika Kipindi cha miezi miwili tangu Taasisi hiyo ipewe jukumu la kusimamia Hospitali hiyo.
Hata hivyo Waziri Ummy Mwalimu amesema kuwa Malengo ya Serikali ni kutanua wigo wa Huduma za Kibingwa hivyo kuitaka Hospitali hiyo kujikita katika utoaji wa huduma za matibabu ya Moyo kwa Watoto wenye umri wa chini ya miaka 15.
Amesema licha ya huduma nyingine kuendelea kutolewa Hospitali hiyo itakuwa imejikita zaidi kwenye umahiri katika Matibabu ya Moyo kwa Watoto.
“Kuna ongezeko kubwa la mahitaji ya matibabu ya Moyo kwa Mkoa wa Dar Es Salaam na nchi nzima kwa ujumla, na pale JKCI kuna msongamano mkubwa wa wagonjwa, wataalam wetu wanafanya kazi kubwa sana lakini matatizo ya moyo yaongezeka siku hadi siku kwa hiyo matibabu ya moyo yakitolewa hapa pia itasaidia kupunguza msongamano JKCI” amesema Waziri Ummy
Hapo awali Hospitali ya Dar Group ilijengwa kwa ajili ya kutoa Huduma za Afya kwa wafanyakazi wa Viwandani na kusimamiwa na Msajili wa Hazina.
Mnamo mwezi Novemba 2022 Serikali kupitia Wizara ya Fedha, Msajili wa Hazina walifanya maamuzi ya kuichukua Hospitali hiyo na kuipatia Wizara ya Afya kwa ajili ya usimamizi na kutatua changamoto za kiutendaji zilizokuwepo hapo awali.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.