WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Doroth Gwajima leo tarehe 6 Septemba, 2021 amezindua magari ya kisasa ya Kliniki Tembezi manne (na la tano lilikwisha tangulia kuwasili na lipo Mkoani Kilimanjaro), pikipiki 160, mashine 50 za uchunguzi za aina ya 'GeneXpert' pamoja na mashine 179 za ECG kwa ajili ya kuboresha huduma za matibabu ya TB na ukoma vilivyogharimu shilingi bilioni 6.2 ambazo zitasaidia kupunguza idadi au kuondoa kabisa wagonjwa wasiofikiwa wanaougulia majumbani hapa nchini.
Dkt. Gwajima amezindua hospitali hizo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma na tukio hilo kuhudhuriwa na baadhi wa viongozi wa Wizara ya Afya, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka, Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Fatma Mganga na wengineo. Lengo la ununuzi wa vitendea kazi hivyo ni kuboresha huduma za matibabu ya ugonjwa wa Kifua Kikuu (TB) na ukoma ili kuutokomeza kabisa hapa nchini.
Waziri Dkt. Gwajima amesema kuwa Serikali kwa kushirikiana na Mfuko wa Dunia wa Kupamabana na Magonjwa ya UKIMWI, Kifua Kikuu na Malaria yaani 'Global Fund ATM' wamefanya ushirikiano mzuri hata kufanikisha ununuzi wa vitendea kazi hivyo.
Naye Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Edward Mbanga amesema kuwa "Wajibu wa Wizara ni kuhakikisha kuwa vifaa hivi vinatunzwa, vinatumiwa ipasanyo na vinaleta tija katika huduma tarajiwa kwa mikoa ambako vinapelekwa."
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.