Na. Dennis Gondwe, MNADANI
WAKAZI wa Kata ya Mnadani wametakiwa kuweka malengo ya kiuchumi kabla ya kuamua kuchukua mikopo kwa lengo la kujikwamua kiuchumi.
Kauli hiyo ilitolewa na Diwani wa Viti maalum Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Joan Mazanda alipokuwa akiongea na wakazi wa Kata ya Mnadani jijini hapa katika ziara ya madiwani hao ya kuchochea maendeleo ya wananchi.
Mazanda alisema “tumekuja kuongea nanyi masuala ya kiuchumi pamoja na mikopo, tumekuja kuongea nanyi masuala ya kupinga ukatili wa kijinsia. Watu wengi wamekuwa wakichukua mikopo na kushindwa kuirejesha kutokana na kutoweka malengo ya matumizi ya mkopo husika. Halmashauri ya Jiji la Dodoma imetoa mikopo mingi ya kuchochea uchumi lakini marejesho yake hayaridhishi. Tumekuja hapa kuwakumbusha kuwa mna wajibu wa kurejesha mikopo ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu ili kutoa fursa kwa wenzenu pia kukopa” alisema Mazanda.
Akiongelea masuala ya ukatili wa kijinsia alisema kuwa suala hilo ni changamoto kubwa. Alisema kuwa jamii inashuhudia ukatili wa kijinsia kwa watoto, wanawake hadi wanaume. “Watoto wamekuwa wakifanyiwa ukatili wa kijinsia, wanawake wamekuwa wahanga wa ukatili wa kijinsia na siku hizi wanaume pia wamekuwa waathirika wa vitendo vya ukatili wa kijinsia. Sisi madiwani wa viti maalum wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma tumekuja kupaza sauti juu ya vitendo vya ukatili wa kijinsia ili watu watumie uhuru wao kufanya shughuli za maendeleo” alisema Mazanda.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.