TAKWIMU zinaonesha takribani watu 10 kati ya 100 wana tatizo la ugonjwa wa Kisukari ambapo asilimia 60 ya wagonjwa wa ugonjwa huo hawajui kama wanaumwa.
Hayo yameelezwa Jijini Dodoma na Mkurugenzi Msaidizi Kitengo cha Magonjwa yasiyoambukiza zkutoka Wizra ya Afya, Maendeleo ya Jamaii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. James Kihologwe wakati akizungumza kwenye mkutano wa Waganga Wakuu na Waratibu wa Magonjwa yasiyoambukiza ambao walitoka katika Mikoa 26.
Dkt. Kihologwe amesema magonjwa ambayo ni ya kuambukiza yawekuwa yakiongezeka nchini na takwimu zinaonesha kwamba watu 26 kati ya 100 wanamatatizo ya shinikizo la juu la damu.
Amesema takribani watu 10 kati aya 100 au asilimia 9 wanatatizo kubwa la kisukari ambapo amedai pamoja na ukubwa huu lakini takwimu zinatuaonesha kwamba takribani asilimia 60 ya wagonjwa huo hawajui kwamba wana tatizo la Kisukali.
Aidha, amesema kuwa watu 36 mpaka 22 wanamafuta mengi katika mishipa yao ya damu ambapo amedai zaidi ya robo tatu ya watu wenye shinikizo la juu la damu hajijui kama wana tatizo hilo.
“Lakini zaidi ya robo tatu ya watu wenye shinikizo la juu la damu hawajijui kama wanatatizo hilo unasikia tu mtu ameanguka hajijui,” amesema.
Mkurugenzi huyo Msaidizi amesema matatizo hayo yamekuwa yakiongoezeka kwa Watanzania hivyo kupunguza maendeleo ya nchi ambapo amedai katika kila asilimia 10 ya ongozeko la magonjwa hayo yamekuwa yakipunguza pato kwa asilimia 0.5.
Amesema kutokana na ongezeko la magonjwa ambavyo sio ya kuambukiza, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imekuja na mpango wa kuhakikisha matatizo hayo yanapungua kwa kuja na mpango wa kubadili mtindo wa maisha ili kukabiliana na magonjwa yasiyoambukiza.
Akifunga mkutano huo, Mkurugenzi wa Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Dkt. Ntuli Kapologwe amesema nchi imekuwa an Mipango mikakati mingi ambapo amedai mingi imekuwa haiwasaisii Watanzania.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.