• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Wenyeviti Serikali za Mitaa Hombolo Bwawani wapewa mafunzo huduma ndogo za kifedha

Imewekwa tarehe: August 6th, 2025

Na. Rehema Kiyumbi, HOMBOLO BWAWANI

Dawati la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Halmashauri ya Jiji la Dodoma latoa elimu kwa wananchi wa Kata ya Hombolo Bwawani juu ya matumizi ya fedha na kuweka akiba kwa lengo la kujikwamua kiuchumi.

Akizungumza na wananchi wa kata hiyo, Mratibu wa Dawati la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Hidaya Abdallah alisema kuwa elimu ya huduma za kifedha ni muhimu kwa wananchi ili kuweza kufahamu namna ya kufanya matumizi na kuweka akiba.

Alisema kuwa kikao hicho kimewahusisha wenyeviti wa serikali za mitaa kwasababu ndio viongozi wa karibu na wananchi. “Hii elimu ya huduma za fedha, tunayowaletea ni mahsusi kwenu kwasababu itawasaidia kufanya maamuzi sahihi wakati wa matumizi. Lakini pia, katika kutunza na kuweka akiba. Huduma ndogo za mikopo ya fedha, mikopo ya vitu na vifaa mbalimbali, mikopo ya nyumba, elimu ya ujasiriamali pamoja na huduma za bima ya afya na bima ya mali ni muhimu kufahamu ili kuwa katika mazingira salama ya kupata au kutoa huduma bora muda wote” alisema Abdallah.

Aliendelea kusema kuwa katika eneo la sera, sheria na kanuni za huduma ndogo za fedha kuna umuhimu wa wananchi kuzifahamu huku akitaja kuwa benki, wakopeshaji binafsi, watoa huduma ndogo za fedha kwa njia ya kidigitali, vyama vya ushirika wa akiba na mikopo (SACCOS) na vikundi vya kijamii kama VSL, SILC na VICOBA ni moja ya watoa huduma ndogo za fedha wanaweza kuwatumia ili kukuza uchumi na biashara zao.
Akizungumza katika kikao hicho, alisema kuwa moja ya umuhimu wa sera hizo ni kumlinda mtumiaji na kuwawezesha wananchi kujiwekea akiba na kupata mikopo nafuu kwa ajili ya kuendesha shughuli mbalimbali za kiuchumi ili kujikwamua na umasikini. 

Aliongeza kuwa pamoja na uwezeshaji bado kuna changamoto wanakutana nazo. “Hata hivyo, mbali na uwezeshaji na usajili kutoka kwa wawezeshaji, bado kumekuwa na changamoto katika usajili kwa wananchi kuwa na hofu ya kupoteza mapato hali inayopelekea kupotea kwa uhuru wa kujiendesha kwa baadhi ya vikundi kuona kuwa kusajiliwa kutawalazimisha kufuata masharti ya serikali na kupoteza uhuru wao wa ndani. Naendelea kuwaasa ninyi viongozi na maafisa maendeleo kuendelea kuwapa elimu wananchi na kuwasilisha chagamoto zao ili ziweze kutatuliwa” aliongeza Abdallah.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Msisi, Yoram Magomba alieleza faida alizopata kwenye mafunzo hayo. “Nashukuru sana kupata mafunzo haya, nikitoka hapa nitaenda kuwaelimisha na wananchi wenzangu ili sote tuweze kuwa na nidhamu ya fedha. Faida ya kusajili vikundi itaenda kuwa chachu ya vikundi kufanya vizuri katika matumizi na kutunza fedha” alisema Magomba.


Imehaririwa na Nancy Kivuyo




Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Serikali yaboresha mazingira ya kufundishia na kujifunza- Mwambene

    August 18, 2025
  • Afisa elimu mkoa wa Dodoma akagua maandalizi ya Juma la elimu ya watu wazima

    August 17, 2025
  • Wafanyabiashara wa mkoa wa Dodoma watangaziwa fursa za biashara nchini indonesia

    August 16, 2025
  • Wafugaji waaswa kufuga kwa kuzingatia uwezo wa malisho ili kupata tija

    August 15, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.