Na. Sifa Stanley, DODOMA
MWAKILISHI wa Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Dkt.Fatuma Mganga atoa wito kwa wananchi wote nchini kuchukua hatua ya kutembelea vyombo vya haki za binadamu ili kupata msaada wa kisheria.
Wito huo aliutoa katika maonesho ya kuadhimisha miaka 20 ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora yaliyofanyika katika uwanja wa Jakaya Kikwete Convention Center jijini Dodoma.
Akiwasihi wanachi kutembelea Taasisi za haki za binadamu alisema kuwa “kuna Taasisi za kutosha za kumsaidia mwananchi tena yule mwananchi wakawaida kabisa katika kupata haki zake, tunamsikia Rais wetu kila siku akisema kuwa vyombo vyote vinavyojishughulisha na utoaji wa haki, vitoe haki na leo nimeshuhudia kuna vyombo vingi vya serikali na taasisi vikijishughulisha na utoaji wa haki. Sasa nichukue fursa hii kuwaasa ndugu zangu na vyombo vyote hebu twende tukaone ufanisi wao kwa matendo, nikisema kwa matendo ni kwamba malalamiko ya wananchi yapungue na tuwasikie wakitoa hongera kuwa wamesaidiwa kupata haki zao” alisema Dkt. Mganga.
Akiongelea juu ya suala la ufuatiliaji wa watu au taasisi zinazowezeshwa ili kutoa huduma kwa wananchi, Dkt. Mganga alisema kuwa ni lazima vyombo hivyo vya msaada wa kisheria kufanya ufatiliaji kujua kama taasisi hizo zinawafikia wananchi ambao ndio walengwa wa huduma.
“Wekeni njia Madhubuti yakuhakikisha mnawafikia wananchi wote na kuwafatilia wale mnaowawezesha kama kweli wanafanya kazi hizo za kuwafikia na kutoa msaada wa kisheria kama taasisi zenu zinavyolenga kufikisha huduma hizi kwa jamii” aliongeza Dkt. Mganga.
Naye Mtapa Wilson, Afisa Mawasiliano wa Taasisi ya “Legal Service Facility” alielezea kuwa taasisi yao hufanya mapitio, tathimini na ufatiliaji wa moja kwa moja kwa wale wanaowawezesha katika kutoa msaada wa kisheria kwa jamii.
“Tunautaratibu wakufanya mapitio, tathimini na ufatiliaji kwa wale tunaowawezesha ili kuona kama kweli msaada wetu unatumika vizuri na kuwafikia wananchi kweli” alisema Wilson.
Maonesho haya ya 20 ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora yanafanyika katika uwanja ua Jakaya Kikwete Convention Center, na yalianza rasmi tarehe 09/09/2022 na kufikia tamati leo tarehe 15/09/2022.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.