KAMATI ya Bunge ya kudumu ya huduma na Maendeleo ya Jamii, imeitaka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum kuwekeza katika ujenzi wa mabweni ya wanafunzi wa kiume kwenye vyuo kama ilivyo kwa wasichana, ili nao waepukane na athari za ukatili unaoweza kuwakumba kwa kuishi nje ya mazingira ya Chuo.
Kamati pia imeitaka Wizara kuratibu suala la uanzishaji wa Madawati ya Jinsia kwenye Vyuo vyake vyote ili kutoa fursa kwa wanafunzi kupata sehemu ya kupazia sauti zao pindi wanapokumbana na madhila ya ukatili wawapo chuoni.
Kamati hiyo ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, imetoa maelekezo hayo mbele ya ujumbe wa Wizara uliokuwa ukiongozwa na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maaalum Dkt. Dorothy Gwajima, wakati wa uwasilishaji wa taarifa ya utekelezaji taarifa ya majukumu ya Chuo cha Maendeleo ya Jamii Uyole kwa robo ya kwanza ya Julai hadi Septemba.
Akizungumza kwenye kikao hicho mara baada ya kupokea taarifa ya Kaimu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Fatma Toufiq alisema kutokana na kushamiri kwa Vitendo vya Ukatili kwa watoto bila kujalisha jinsi zao ameitaka Wizara pia kujielekeza katika ujenzi wa mabweni ya wavulana kwa kuwa nguvu kubwa ya uimarishaji wa miundombinu ya mabweni ilikuwa imeelekezwa kwa wasichana zaidi.
"Mwanzoni ilionekana watoto wa kike ndio wapo katika athari kubwa ya Ukatili hivyo nguvu ya kujenga mabweni ilielekezwa kwao na kuwasahau watoto Kiume hivyo ni wakati sasa kulikumbuka kundi hilo" alisema Fatma
Mbali na maelekezo hayo Kamati pia haikusita kuipongeza Wizara kwa jitihada hizo za uimarishaji wa Miundombinu katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii Uyole.
Awali akitoa taarifa mbele ya Kamati hiyo, Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maaalum Dkt Dorothy Gwajima, aliiambia Kamati hiyo kuwa Wizara imeendelea
kuimarisha mazingira ya kujifunza na kufundishia kwa Vyuo vyake vyote ikiwepo cha Uyole kinachoendelea na Ujenzi wa bweni la wasichana litakaloweza kuchukua wanafunzi 600.
Chuo cha Maendeleo ya Jamii Uyole kilianzishwa mwaka 1971 kikiwa na lengo la kutoa Mafunzo ya Maendeleo ya Jamii.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.