WAZIRI MKUU wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb) ameziagiza Wizara zote za Serikali zilizopo Dodoma zinazotumia magari yake kusafirisha vifurushi na nyaraka mbalimbali kutumia Shirika la Posta Dodoma.
Mhe. Majaliwa aliyasema hayo jana alipokuwa akijibu ombi la Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Faustin Ndugulile kwenye hafla ya uzinduzi wa Vituo vya Huduma Pamoja ambapo Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa alikuwa Mgeni Rasmi.
"...Wizara zote ziko Dodoma, Shirika la Posta Dodoma linatoa huduma, sasa elekezeni kwenye Shirika la Posta pale kusafirisha vifurushi hivyo... iwe vinaenda Mwanza, Morogoro, Arusha, kuja Da es Salaam, tumia shirika la Posta, Makatibu Wakuu mko hapa mnanisikia.
Baneni matumizi ya kutumia magari na posho na kupunguza pia 'risk' za magari hayo. Nenda tu pale Shirika la Posta kupata huduma. Kutoka Mtumba mpaka Posta si mbali." Alisema kwa mkazo Waziri Mkuu Majaliwa.
Shirika la Posta Tanzania limeanzisha Vituo vya Huduma Pamoja katika matawi yake ya Dar es Salaam na Dodoma ambapo huduma mbalimbali zinazotolewa na taasisi za Serikali zinapatikana. Lengo ni vituo hivi kuwepo kila mkoa ifikapo mwaka 2025.
Taasisi ambazo tayari zimeanza kutoa huduma zao katika kituo cha Dodoma (Posta) na Dar es Salaam ni Halmashauri ya Jiji la Dodoma, RITA, NIDA, PSSF, NSSF, NHIF, TRA, Uhamiaji, Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Benki ya CRDB, BRELLA na Posta yenyewe,.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.