WIZARA ya Afya Maendenleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, imepanga kukamilisha jengo la ghorofa tisa ndani ya miezi 24 ambalo litakuwa na uwezo wa kuchukua watumishi 400, imebainishwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Wtoto, Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima wakati wa zoezi la kusaini mkataba wa ujenzi na kukabidhiana eneo la ujenzi katika eneo la Mtumba, mji wa Serikali mwanzoni mwa wiki hii.
Akiongea wakati wa hafla fupi ya kusaini mkataba huo, Novemba 02, 2021 Dkt. Gwajima amesema makubaliano baina ya Wizara na Mkandarasi Nandhra wa mjini Morogoro, yamekuja baafa mara baada ya Serikali ya Rais wa awamu ya sita Mhe. Samia Suluhu Hassan kutoa fedha kiasi cha bilioni 23 kwa ajili ya ujenzi wa jengo hilo la Wizara ambalo litajumuisha Idara kuu Afya ya Jamii Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii na kwamba, ni imani mradi utaanza kwa wakati na kukamilika ndani ya miezi 24 kama ilivyopangwa.
"Hatutegemei kipindi cha miezi 24, kipite kama maelekezo ya Serikali yalivyotaka halafu kazi iwe haijakamilika, niimani yetu Mkandarasi atakuwa na mpango kazi utakaoainisha kila siku nini kitakuwa kinafanyika" Amesema Waziri Gwajima.
Dkt. Gwajima ameitaka Idara ya Tathmini na Ufuatiliaji ndani ya Wizara kutowaachia kazi Mkandarasi na kukaa pembeni badala yake waweke kadi ya maendeleo ya (score card) ya ujenzi na iwe inakaguliwa kila jumatatu ili kubaini maendeleo ya ujenzi, huku akihimiza viongozi wa Wizara kufanyia vikao vyao eneo la ujenzi (site meetings).
Kwa upande wao Wakala wa Ujenzi Nchini (TBA), ambaye ni Mkandarasi Mshauri, amemhakikishia Mhe. Waziri na ujumbe wake kuwa, Mkandarasi huyo, watamsimamia ili kuhakikisha anakamilisha kazi hiyo ndani ya kipindi ambacho kimepangwa au chini ya hapo, huku akisema anaimani na Mkandarasi Nandhra kutokana na uzoefu wake.
"Mhe. Waziri Mkandarasi aliyepewa jukumu hili, anafahamika kwa sifa yake ya kuwa mkandarasi daraja la kwanza, tunaimani kabisa, kazi hii itakamilika kwa wakati kama ilivyopangwa." Alisema Msanifu Majengo Wencelaus Kizaba kutoka TBA, na kuongeza kuwa , tayari taasisi hiyo imepeleka wataalam 17 katika eneno hilo la Mtumba.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.