KATIKA kuhakikisha msingi wa Sera ya Afya ya mwaka 2007 kwamba "KINGA NI BORA KULIKO TIBA" inazingatiwa, Wizara ya Afya imeamua kubeba jukumu la kusimamia Usafi wa Mazingira moja kwa moja kupitia Idara ya Kinga ili kuepukana na magonjwa ya mlipuko.
Akizungumza jijini Dodoma, wakati wa kilele cha Wiki ya Usafi wa Mazingira Kitaifa na Siku ya Matumizi wa Choo Duniani na utoaji wa tuzo za Usafi, Naibu katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt.Seif Shekalaghe amesema kuwa,usafi wa mazingira kwa ujumla wake unachangia kwa sehemu kubwa kuzuia magonjwa ya kuambukiza na yasiyoambukiza.
"Kwa kuwa leo ni kilele cha Wiki ya Usafi wa Mazingira nchini, napenda kuikumbusha jamii umuhimu wa kuweka mazingira katika hali ya usafi,Sote ni mashahidi kwamba, hali ya usafi katika maeneo mengi bado si ya kuridhisha sana,atika baadhi ya maeneo udhibiti wa taka ngumu na majitaka haufanyiki kwa kiwango cha kuridhisha na hivyo kupelekea kuwepo kwa uchafu uliokisiri hali inayohatarisha afya ya jamii,
Na kuongeza kuwa " Kutokana na msingi huu, Serikali kupitia Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa imeunda Kitengo katika Halmashauri zote kusimamia suala la Udhibiti wa Taka na Usafi. Kitengo hiki kina jukumu la kusimamia shughuli zote za usafi wa mazingira katika Halmashauri.
Wizara ya Afya kupitia vitengo hivi imebeba jukumu la kutoa Miongozo ya Kisera kwenye Kitengo hiki ili kiweze kutekeleza vema majukumu yake kwani madhara ya uchafu huigusa sekta ya afya zaidi pengine kuliko sekta nyingine yoyote, Mfano, kunapotokea magonjwa ya mlipuko kama vile, kipindupindu, kuhara na kuhara damu sekta ya afya ndio hubeba jukumu kwa sehemu kubwa kukabiliana na milipuko ya aina hii," Amesema Dkt.Shekalaghe
Dkt. Shekalaghe amedokeza kuwa, uwepo wa vyoo bora kwa upande wa kaya umeongezeka sana katika kipindi cha miaka kumi iliyopita ambapo kwa sasa vyoo bora katika ngazi ya kaya umeongezeka kutoka asilimia 19.5 mwaka 2012 hadi kufikia asilimia 72.6 mwaka 2022,huku Kaya zisizokuwa na vyoo kabisa
zimepungua kutoka asilimia 20.5 hadi kufikia asilimia 1.4 sasa.
Aidha, Dkt. Shekalaghe amesema kwa ujenzi wa vyoo bora pamoja na uwepo wa huduma za maji safi na salama umeongezeka.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.