WIZARA ya maendeleo ya jamii imetoa mafunzo ya masuala mtambuka ya Ustawi wa Jamii kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, jijini Dodoma.
Akiongoza mafunzo hayo, Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe Mwanaidi Ali Khamis amesema ni wakati muafaka kwa Wajumbe wa Kamati hiyo kuwa na uelewa mpana wa masuala ya ustawi wa jamii ili waweze kuyasemea kwa nguvu zote.
Baadhi ya masuala waliojifunza wajumbe wa Kamati hiyo ni pamoja na masuala ya Watoto, Wazee, pamoja na afua zinazotumika kushughulikia masuala yanayo wahusu.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Fatuma Toufiq amesema, mafunzo kama hizo ni muhimu hasa ikizingatiwa kuwa kamati hiyo ina jukumu la kuishauri Wizara katika masuala hayo.
Kwa Upande wao Wabunge, Wameipongeza Wizara kwa jitihada wanachukua katika kukabiliana na Masuala ya Ukatili lakini pia mbinu anuwai wanazo tumia kuchechemua masuala ya Maendeleo.
Katika hatua nyingine Wabunge hao waliomba kuangalia mwenendo wa sheria zinazo wahusu watoto wanao kinzana na Sheria na kufanyia maboresho.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.