WIZARA ya Maji imepanga kukutana na wadau wanaotumia maji ili kuweka mfumo mzuri wa ushirikiano na kuepuka changamoto mbalimbali.
Waziri ya Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) amesema hayo na kuwakumbusha watumia maji wote wa Bonde la Usangu kuzingatia Sheria ya Usimamizi wa Rasilimali za Maji Namba 11 ya mwaka 2009 na marekebisho yake ili kuepuka madhara ya kubomolewa miundombinu.
Aweso ameyasema hayo leo akiwa na Mawaziri wa Kisekta katika ziara maalumu ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa alipofanya ukaguzi kuhusu hali ya hifadhi ya Usangu, Ranchi ya Usangu, Ihefu, Madibila, Ubaruku na Kapunga na baadae kuzungumza na wanachi katika eneo la Kapunga.
Ukaguzi huo unatokana maamuzi ya Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufanya marekebisho kwenye tangazo la Serikali namba 28 ambalo limetoa hekta 74,000 kwa wananchi kwa ajili ya shughuli za kilimo na ufugaji endelevu ambapo leo Waziri Mkuu ametoa tamko rasmi la serikali la kufuta GN 28 lililoanisha mpaka wa Hifadhi ya Taifa ya Ruaha.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.