• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Wizara yajikita kutoa elimu ya malezi kwa vijana balehe

Imewekwa tarehe: October 8th, 2024

Na WMJJWM Singida

Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum inaendelea na mkakati wake wa kuwajengea uwezo wa kutoa elimu mahsusi ya malezi na uzazi kwa vijana balehe Maafisa Maendeleo ya Jamii, Maafisa Ustawi wa Jamii na waratibu wa Afya ya Mama na Mtoto wa mikoa mbalimbali kwa lengo la kutoa elimu kwa vijana balehe wengi ili kuboresha malezi katika familia na Taifa.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Mtoto kutoka Wizara hiyo Asha Shame wakati akifungua mafunzo ya siku tatu yanayofanyika mkoanj Singida kuanzia Oktoba 07-09, 2024.

Asha amesema Wizara itaendelea kutoa elimu hiyo itakayochochea mabadiliko ya fikra za wazazi na walezi katika kujenga jamii ya watoto wenye malezi bora, maadili na wenye tija kwa maendeleo ya taifa kwani elimu ya malezi inaanza kwenye familia ambapo familia ni chanzo cha Jamii yeyote ile duniani.

“Niseme lengo kuu la mafunzo haya ni kujengeana uwezo kuhusu elimu ya malezi na uzazi kwa vijana belehe. Tunafahau kuwa Familia ni chimbuko la tabia, mwelekeo na mtazamo wa mtu binafsi na jamii kwa ujumla katika maendeleo ya kijamii, kiutamaduni na kiuchumi. Vile vile, familia ni chimbuko la maadili ya kitaifa na uzalendo katika kudumisha umoja, amani na mshikamano.” amesema Asha.

Ameeleza Mwongozo wa Wajibu wa Wazazi/Walezi katika malezi na Matunzo ya Watoto na Familia ni jawabu la changamoto za malezi ya watoto zilizoibuliwa kupitia tafiti shirikishi kati ya wadau wa malezi iliyofanyika mwaka 2015 ambapo ilibainika wazazi wengi hasa wa kiume wamekuwa hawawajibiki kwenye malezi ya watoto na kupelekea jukumu hilo kubebwa na wazazi wa kike katika maeneo yote ya mjini na vijijini.

Aidha, amesema baada ya mafunzo hayo wawezeshwaji watakuwa na uwezo wa kupata mbinu zitakazowawezesha kufikia jamii kuanzia ngazi ya kaya pamoja na wadau muhimu katika malezi ya watoto wakiwemo viongozi wa dini, wazee wa mila na vyombo vya habari, Kupata elimu ya mnyororo chanya wa malezi ya watoto kuanzia kipindi cha utungaji wa mimba mpaka vijana balehe kupitia nguzo kuu tatu zilizoainishwa kupitia Mwongozo wa Wajibu wa Wazazi na Walezi.

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.