• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Yaliyojiri kikao cha JPM na Watendaji wa Kata jana Ikulu Dar es salaam

Imewekwa tarehe: September 3rd, 2019

Dondoo za Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa Watendaji wa Kata takribani 3,800 nchini aliowaita Ikulu jijini Dar es salaam jana 02 Septemba, 2019:-

  • Nawahakikishia kuwa cheo cha Afisa Mtendaji Kata siyo kidogo, ninyi ni wawakilishi wangu na nawahakikishieni tembeeni vifua mbele na kamwe asitokee mtu wa kuwanyanyasa huko mliko.
  • Nimewaita tusalimiane, tujadiliane namna bora ya kutimiza wajibu wenu katika maeneo yenu mnakotoka, sina hakika katika maisha yenu kama mmeshawahi kuitwa na Wakuu wa Wilaya ama Wakurugenzi wa Halmashauri, kujadili kwa pamoja utendaji kazi wenu.
  • Najua mmekua mkionewa, mmekua mkihamishwa hovyo hovyo kwa utashi wa wakubwa wenu na nasema ni marufuku kwa Afisa Mtendaji Kata kuhamishwa bila kufuata taratibu.
  • Hiki ni kikao muhimu sana ndiyo maana nataka tuzungumze na kujadiliana juu ya utekelezaji wa majukumu yenu ya kila siku kwakua ninyi ndiyo mko karibu na wananchi na hakuna anayezielewa na kuzijua changamoto za Vijiji na Kata nchini zaidi yenu.
  • Mna majukumu ikiwemo kuhakikisha usalama katika maeneo yenu, amani ndiyo msingi wa maendeleo lakini nasistiza hususani kwa kata zilizoko mpakani, watambueni wageni wanaoingia mipakani na hakikisheni hawapati vitambulisho vya uraia ambavyo zoezi la kuvitoa kwa wananchi linaendelea.
  • Kutatua kero za wananchi ni jukumu lenu lingine, jiwekeeni utaratibu wa kukutana na wananchi na siyo kusubiri wananchi wabebe mabango wakati wa ziara ya Rais na kama hamtasikiliza na kutatua kero za wananchi uwepo wenu katika maeneo yenu hautakua na maana.
  • Kusimamia miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika kata zenu ni jukumu lenu na kamwe msikubali mradi kutekelezwa chini ya kiwango kwani na wewe utahusika, wewe ni bosi hupaswi kukaa pembeni wakati pesa zinachezewa.
  • Natoa rai kwa baadhi yenu, taarifa ninazo acheni kua madalali wa  kuuza ardhi kwani ndio chanzo cha migogoro ya ardhi nchini, acheni kujihusisha na vitendo vya rushwa na dhuluma, mnabambikia wananchi kesi, hamna huruma hata kwa wajane na yatima.
  • Siku zote mtangulizeni Mungu, mnaposhughulika na maisha ya wananchi, mkumbuke maisha mliyoanza nayo.
  • Nitasikitika sana baada ya kikao hiki Afisa niliyemteua akaenda kumnyanyasa kwa makusudi Afisa Mtendaji Kata nitamuona hatoshi  lakini pia nitashangaa Mtendaji Kata kuwaonea wananchi wanyonge pia nitamuona hatoshi lakini tukumbuke kua hakuna mkubwa kuliko mwingine sisi wote ni sawa.
  • Najua kuna watu hawakufurahishwa ninyi kuitwa na mimi na kuna baadhi yenu mmetendewa isivyofaa.
  • Maneno ninayoyasema najua hayatawafurahisha  wakubwa wenu ila mimi ndiyo mkubwa wenu wote na sababu kubwa ya kuwaita hapa ni kuwapa meno na kujitambua kuwa ni mabosi, tembeeni kifua mbele.

Dkt. Laurean Ndumbalo, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma alisema:-

  • Mambo makubwa matatu mnayopaswa kuyatekeleza katika maeneo yenu ni moja; kuisoma, kuielewa na kuitafsiri kwa vitendo Ilani ya Chama cha Mapinduzi mfano tunaposema Elimu bure, hakikisheni katika maeneo yenu watoto wote wanaopaswa kwenda shule wanakwenda.
  • Wajibu wenu wa pili ni kutembelea wananchi, kusikiliza kero za wananchi katika maeneo yenu na kuzitatua lakini kwa zile zilizo nje ya mamlaka yenu zipelekeni ngazi inayofuata.
  • Jukumu lenu la tatu ni kuisemea Serikali ninyi mnapaswa kuyasemea yale yanayotekelezwa na Serikali kwa mfano mna wajibu wa kuwaambia wananchi katika maeneo yenu juu ya mambo makubwa yanayofanywa na Serikali mfano katika suala zima la miundombinu ikiwemo ya usafiri na usafirishaji, ujenzi wa barabara katika ngazi ya Miji, Wilaya na Mikoa kama ile inayounganisha mikoa ya Kigoma, Katavi na Rukwa, kuna miradi kama ule wa Flyover na madaraja jijini Dar es Salam.
  • Kuna Ujenzi wa Meli mpya katika ziwa Ziwa Victoria, Nyasa na Tanganyika lakini tayari makandarasi wako kazini  kuanza Ujenzi wa daraja la Kigongo Busisi.
  • Yasemeeni makubwa yanayofanywa katika sekta mbalimbali ikiwemo Afya, Elimu, mambo mengine mengi. Serikali inatoa bilioni 450 kila mwaka kwa ajili ya mikopo ya Elimu ya juu na kubwa zaidi sasa wanafunzi wana uhuru wa kuchagua vyuo wanavyotaka kwenda kwa sifa  stahiki tofauti na miaka ya nyuma ambako walikua wanalazimishwa kwenda TCU walikokua wanataka jambo ambalo Rais Magufuli alilikataa.
  • Mambo ni mengi tutakesha nikisema niyaorodheshe lakini waambieni kuhusu ujenzi wa reli ya kisasa (SGR), upatikanaji wa dawa ambapo Serikali imeongeza bajeti ya afya kutoka shilingi Bilioni 31 mpaka Bilioni 270 ili kunusuru maisha ya Watanzania, vituo vya afya 300 vimejengwa na Hospitali 67 zimejengwa kwa wakati mmoja katika kipindi cha miaka mitatu ya Rais Magufuli na Serikali ya Awamu ya Tano, waambieni kuhusu kufufuliwa kwa Shirika la Ndege la ATCL, ndege sita tayari zimenunuliwa kwa fedha zetu wenyewe na nyingine mbili zinatarajiwa kuja kabla ya mwisho wa mwaka huu.

Chanzo: Idara ya Habari MAELEZO



Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.