Rais Daktari John Pombe Magufuli:
Ndugu Watanzania, Kukaa meza ya Mazungumzo na Kigogo hiki Barrick, chenye msuli mkubwa wa uwezo na Ushawishi, haikua kazi rahisi.
Nampongeza sana Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Paramagamba Kabudi, aliyeongoza timu ya Wataalamu Wazalendo kufanikisha jambo hili.
Mazungumzo hayo yalichukua miaka mitatu yakianzia mwaka 2017 mpaka leo tunapotia saini makubaliano baina yetu na Barrick.
Mkasimamie vyema makubaliano haya na kwenu Wizara ya Madini, Nawaomba kuhakikisha Watanzania watakaopewa dhamana kwenye Kampuni ya pamoja baina ya Tanzania na Barrick ya Twiga Mineral Corporation, kuhakikisha kuwa Wanaangalia maslahi ya nchi na si yao binafsi.
Naweza kusema kuwa Majadiliano haya yalikua ni vita ya Tembo na Sungura, lakini kwa hatua ya leo ni sawa na kusema vita imeisha kwakua lengo lilikua pande zote kufaidika na wamekubali.
Profesa Palamagamba Kabudi:
Kubwa katika Mazungumzo yetu tulikubaliana kuunda kampuni ya Twiga Mining Corporation, ambayo Barrick atakua ni mbia ndani ya kampuni hiyo.
Watanzania muelewe kuwa Serikali itashiriki maamuzi ya kila kitu katika kampuni hiyo ya Twiga Mineral Corporation, ambayo Serikali itakua na hisa za asilimia 16 na siyo Twiga tu bali asilimia 16 kwa migodi yote.
Nyie Barrick Ondoeni Mtazamo kua kuna Barrick Tanzania bali ni mbia wa Twiga Mineral Corporation iliyoundwa Septemba 10, 2019.
Mark Bristow - Rais na Mtendaji Mkuu Barric:
Mheahimiwa Rais, hii ni siku ya kipekee barani Afrika, tuna furaha kuanza upya ushirika wetu, tunakubali kuwa awali kulikua kuna tatizo mashaka, lakini sasa tuko tayari kuwa na mwanzo mpya wenye faida kwa pande zote.
Kuna baadhi ya Watanzania, walivumisha kuwa eti Tanzania inataka kuwakera wawekezaji, siyo kweli na niko hapa kuwahakikishia kuwa huo ni uzushi na kwamba inachokifanya Tanzania, ni kitu chema kwa maslahi ya Watanzania.
Picha za matukio mbalimbali wakati wa hafla hiyo:
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.