Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile.
Katika mwaka 2017/2018, Wizara kwa kushirikiana na Wadau wa Maendeleo, ilitenga kiasi cha TShs. Bilioni 2 zilizotumika kusomesha Madaktari Bingwa 125 wa Fani ya Kipaumbele chuo cha MUHAS.
Katika mwaka 2018/19, Serikali ilitenga kiasi cha Shilingi Bilioni 1.8, ili kuendelea kugharamia mafunzo ya ngazi ya Kibingwa katika kada mbalimbali za afya 127 Katika chuo cha MUHAS.
Hadi kufikia mwezi Juni 2019, jumla ya watumishi wa sekta ya afya 458 walikuwa wanaendelea na masomo katika ngazi mbalimbali za taaluma. Watumishi 435 wanaendelea na masomo yao ndani ya nchini na 23 nje ya nchi kwa ufadhili wa Serikali.
Jumla ya Madaktari Bingwa 365 wanatarajia kuhitimu mafunzo yao kuanzia mwaka wa masomo 2019/2020, 2020/2021 na 2021/2022 ambapo watasambazwa kwenye hospitali mbalimbali nchini kulingana na uwiano wa wataalamu waliopo pamoja na kuzingatia maeneo yenye uhaba mkubwa.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji.
Benki ya TPB imefanikiwa kujitangaza na kuimarisha huduma zake na hivyo kuvutia baadhi ya Taasisi za Serikali na Mashirika ya Umma kutumia bidhaa zake.
Miongoni mwa huduma za Benki ya TPB zinazotumiwa na Taasisi za Serikali na Mashirika ya Umma kwa sasa ni pamoja akaunti ya muda maalumu, akaunti ya biashara, malipo kwa njia ya mtandao, kubadilisha fedha za kigeni, kukusanya mapato ya Serikali, kulipa mishahara ya watumishi, mikopo ya watumishi, kulipa pensheni za wastaafu pamoja na mikopo ya wastaafu wanaolipwa pensheni zao na Serikali pamoja na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.
Kwa mujibu wa sera, sheria, kanuni, taratibu na miongozo iliyopo ya uchumi huria, Serikali haina mamlaka ya kumlazimisha mtumishi au Taasisi ya Umma kutumia huduma za Benki yoyote, ikiwemo Benki ya TPB.
Ni jukumu la Benki ya TPB na Benki nyingine kuboresha mifumo ya huduma na bidhaa zao ili kuvutia watumishi wa Umma pamoja na Taasisi za Umma kuanza au kuendelea kutumia huduma zao.
Chanzo: Idara ya Habari - MAELEZO.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.