UONGOZI wa Zahanati ya Nala umetakiwa kujipanga kuwatembelea wananchi katika maeneo yao na kuwaelimisha ili waweze kuchanja chanjo dhidi ya ugonjwa wa UVIKO-19 unaosababishwa na virusi vya Korona.
Kauli hiyo ilitolewa na Afisa Muuguzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Situ Muhunzi (aliyekaa kushoto pichani juu) alipoongoza timu ya wataalam wa Afya wa Jiji la Dodoma kutembelea Zahanati ya Nala jijini Dodoma.
Muhunzi alisema kuwa uongozi wa zahanati hiyo unatakiwa kujipanga vizuri na kuwafuata wananchi katika maeneo yao kuwaelimisha juu ya chanjo ya ugonjwa wa UVIKO-19 ili wafanye maamuzi baada ya kuwa na elimu ya kutosha. “Niwashauri kutoka na kuwafuata wananchi katika maeneo yao na kuwaelimisha. Wale watakao kubali kuchanjwa kwa hiari wachanjwe hukohuko. Utaratibu huu ni mzuri kwa sababu utawaondolea adha wananchi ya kufuata chanjo kituoni hapa” alisema Muhunzi.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.