MBUNGE wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh.Anthony Mavunde ameendelea na ziara za kusikiliza kero za wananchi sambamba na kuhamasisha ushiriki wa zoezi la sensa tarehe 23.08.2022.
Siku ya Jana Mh. Mavunde alikuwa katika kata ya Ihumwa akiongozana na Diwani wa kata ya Ihumwa Mh. Edward Magawa na kufanya mkutano wa hadhara ambapo katika kujibu hoja za wananchi mambo yafuatayo yaliwawasilishwa na Mbunge Mavunde kuyatolea ufafanuzi na majawabu ambayo yameleta matumaini makubwa kwa wananchi katika utatuzi wa changamoto zao zikiwemo:-
Kuanzisha ujenzi wa Shule mpya ya Msingi ya Ilolo ili kuwapunguzia mwendo watoto wa shule wanaotembea umbali mrefu kufuata shule katika eneo la Ihumwa. Pia alitoa ahadi ya Tsh 25,000,000 kwa ajili ya Ujenzi wa Jengo la Kliniki ya Mama na mtoto.
Aidha, Mavunde alizungumzia kuhusu uchimbwaji wa kisima kirefu cha Maji kupitia DUWASA ili kutatua changamoto ya upatikanaji maji safi na salama.
Vile vile, ahadi ya kupeleka mtambo wa kukwangua barabara ya kutoka Ihumwa-Ilolo na kukamilisha zoezi la usambazaji umeme linaloendelea kupitia mradi wa Peri Urban.
Aidha, kupitia mkutano huo wananchi wa Ilolo-Ihumwa wamemshukuru sana Mh. Rais Samia Suluhu Hassan kwa utekelezaji wa miradi mingi ya huduma za kijamii katika maeneo ya Elimu, Afya na Maji na kuonesha imani kubwa na serikali ya awamu ya sita katika kuwahudumia wananchi.
Sensa kwa maendeleo ya Taifa, jiandae kuhesabiwa.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.